Posts

VYAKULA VITAKAVYOKUONGEZEA KINGA YA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA CORONA ( COVID-19)

Image
VYAKULA VITAKAVYOKUONGEZEA KINGA YA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA CORONA ( COVID-19)  Njia za kufuata ili kuimarisha kinga ya mwili ili kupambana na maambukizi ya virusi vya corona Kwa kutambua umuhimu wa kuchukua tahadhari ya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona, nimeamua kutumia jukwaaa hili kufafanua mambo machache kuhusu kinga ya mwili (body immunity) na makundi machache ya vyakula vinavyopatikana kwa urahisi ambavyo vinauwezo wa kuongeza na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili( body immune system). Twende pamoja; 1. Hiriki Mbali na kiungo hiki kutumika kuongeza radha katika vyakula na vinywaji, hiriki ni chanzo kizuri cha madini muhimu mwilini. Madini haya ni kama vile potassium, calcium, madini ya chuma na manganese. Madini haya husaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mapafu na kuzibua mirija ya hewa, hivyo kuwapa unafuu watu wenye matatizo ya pumu na kupumua. Pia hiriki ina vitamini mbali mbali kama vile vitamin A, B na C amb...

KIAFYA: HAISHAURIWI KUFANYA YAFUATAYO BAADA YA KULA CHAKULA:

Image
1.Kuvuta sigara Kiafya mara baada ya kula chakula hairuhusiwi kuvuta sigara japo kuwa mvutaji wa siagara hupatwa na hamu kubwa ya kuvuta mara baada ya kula tabia hii huhatarisha afya, hivyo inashauriwa kusubiri angalau kwa masaa kadhaa ndipo uvute endapo ni lazima sana kwani sigara ina miliki Nikotini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, madhara yanayotokea kwa kuvuta sigara mara baada ya kula chakula ni sawa na madhara yanayotokea kwa mtu aliyevuta sigara 10 kwa mara moja na hii huchangia mtu kupata kansa ya mapafu. 2. Kula matunda Wanasayansi wamedhihirisha kuwa kiafya matunda yanatakiwa kuliwa kabla ya kula si mara baada ya kula kama ambavyo imezoeleka kwa watu wengi, Matunda yana enzymes na asali asili ambayo inahitaji kumeng’enywa ndani ya muda wa kutosha, hivyo kula matunda baada ya chakula inaweza kusababisha matatizo ya mmeng’enyo wa chakula pamoja na kiungulia. 3. Kulala Kulala mara baada ya kula ni kitendo ambacho hupendelewa kufanywa na mamilioni ya watu japokuwa tabia hii s...

FAHAMU JINSI YA KUTENGENEZA SCRUB

Image
FAHAMU JINSI YA KUTENGENEZA SCRUB Habari zenu wapendwa. Leo nimewaletea somo la utengenezaji scrub ukiwa nyumbani kwako na kwa mahitaji rahisi Sana yanayopatikana nyumbani kwako.

KISA CHA MFUGAJI NA FARASI WAKE.

Image
Mfugaji mmoja alikuwa anafuga farasi na kondoo, alimtumia farasi kwa usafiri wake.  Siku moja farasi wake aliugua akaamua kumtafuta daktari wa mifugo amtibu haraka. Daktari wa mifugo akajaribu kumpatia dawa, akamwambia mfugaji kuwa ile dawa lazima iwe imemtibu farasi ndani ya siku 5 na kama zitafikia siku 5 hajapona basi itabidi achinjwe maana ni ishara tosha kuwa hatapona tena sababu ya mashambulizi makubwa ya bakteria. Daktari Akaondoka kwa ahadi ya kurudi tena kuangalia maendeleo ya farasi.  Kondoo alikuwa pembeni akisikiliza kwa makini mazungumzo yao.  Siku ya pili ilipofika, kondoo akamfuata farasi akamwambia "jitie nguvu rafiki yangu amka kama sivyo watakuchinja." Lakini farasi hakuwa na nguvu, alishindwa kabisa kuamka. Ikafika siku ya tatu, kondoo akarudia tena kumwambia : "Amka rafiki. yangu, sitaki kuona unachinjwa, jikaze na mimi nitakusaidia kukushika usianguke, haya twende! Moja mbili tatu….." Jitihada za kondoo zikawa bure maana farasi hakuwez...

ZIFAHAMU FAIDA ZA NJEGERE KIAFYA

Image
ZIFAHAMU FAIDA ZA NJEGERE(GREEN PEAS) KIAFYA Njegere ni moja ya mmea mithili ya maharage ambayo hutumika kama mboga hasa ikiwa mbichi, rangi yake ni kijani. FAIDA ZAKE 1. HUZUIA MWILI USISHAMBULIWE NA MAGONJWA SUGU. Njegere huwa na virutubisho na nyuzi (fibres). Hivyo magonjwa kama kansa, magonjwa ya moyo na kisukari hukosa upenyo wa kushambulia mwili

UMUHIMU WA KOKOTO KUTANDAZWA KWENYE RELI

Image
Kusafiri ndani ya treni (garimoshi) kuna  upekee wake. - Moja ya kitu cha  pekee utakachokiona ni mawe madogo madogo(kokoto) kuzunguka reli ambapo treni inapita. - Lakini umewahi kujiuliza kwanini reli imetandazwa kokoto hizo? 1- Mawe ya relini yanafanya kazi nyingi. Kwanza kabisa, yanasaidia reli kukaa mahali pake wakati treni yenye uzito mkubwa ikiwa inapita - 2- Pia yanazuia aina yoyote ya majani yasiote karibu na reli ambayo yanaweza kuufanya udongo uliopo chini ya reli kuwa dhaifu na kushindwa kuhimili uzito wa reli na treni - 3- Kazi nyingine muhimu inayofanywa na mawe ya relini ni kuzuia maji yasikusanyike au kukaa muda mrefu kwenye reli na kudhoofisha njia ya reli - Hivyo basi ni jukumu letu sote kulinda na kuhakikisha mawe hayo hayaondolewi kwenye reli kwasababu yamewekwa kwasababu maalumu ya kuimarisha reli na kuwalinda watu wanaotumia usafiri wa treni...

FAIDA 28 ZA MAPERA NA MAJANI YAKE

Image
FAIDA 28 ZA MAPERA NA MAJANI YAKE Mapera ni matunda yanayopatikana kwa wingi lakini mara nyingi huwa hayapendwi sana kutokana na ugumu wake wakati wa kuyatafuna pamoja na kuwa na mbegu mbegu nyingi. Hata hivyo matunda haya yana faida kubwa sana kwa afya ya mwili wa mwanadamu. ZIFUATAZO NI FAIDA KUMI ZA MAPERA. 1. Utajiri wa Vitamin C: Mapera ya utajiri mkubwa wa Vitamin C ambayo ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. 2. Ni kinga nzuri ya kisukari. Ulaji wa watu wengi unawaweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari lakini matumizi ya mapera yatakupunguzia hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari Hii ni kwa sababu mapera yana utajiri mkubwa sana wa Fibre. Fibre ni muhimu sana katika kupunguza kiasi cha sukari kwenye damu. Vilevile ni muhimu sana katika kuusafisha mfumo wa usagaji 3. Kuimarisha Uwezo Wa Kuona Mapera yana utajiri mkubwa sana wa Vitamin A au Retinol ambayo ni muhimu sana katika kusaidia kuona vizuri. Hivyo basi kama ilivyo kwa karoti, mapera ...

adthis