FAIDA 28 ZA MAPERA NA MAJANI YAKE
FAIDA 28 ZA MAPERA NA MAJANI YAKE
Mapera ni matunda yanayopatikana kwa wingi lakini mara nyingi huwa hayapendwi sana kutokana na ugumu wake wakati wa kuyatafuna pamoja na kuwa na mbegu mbegu nyingi. Hata hivyo matunda haya yana faida kubwa sana kwa afya ya mwili wa mwanadamu.
ZIFUATAZO NI FAIDA KUMI ZA MAPERA.
1. Utajiri wa Vitamin C:
Mapera ya utajiri mkubwa wa Vitamin C ambayo ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu.
2. Ni kinga nzuri ya kisukari.
Ulaji wa watu wengi unawaweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari lakini matumizi ya mapera yatakupunguzia hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari Hii ni kwa sababu mapera yana utajiri mkubwa sana wa Fibre.
Fibre ni muhimu sana katika kupunguza kiasi cha sukari kwenye damu. Vilevile ni muhimu sana katika kuusafisha mfumo wa usagaji
3. Kuimarisha Uwezo Wa Kuona
Mapera yana utajiri mkubwa sana wa Vitamin A au Retinol ambayo ni muhimu sana katika kusaidia kuona vizuri.
Hivyo basi kama ilivyo kwa karoti, mapera yanasaidia sana katika kuongeza na kuimarisha uwezo w a mtu kuona.
4. Kusaidia katika Uzazi
Mapera yana madini yaitwayo Folate ambayo husaidia katika kurutubisha mayai ya uzazi..
5. Kurekebisha Kiwango Cha Shinikizo La Damu
Madini ya Potassium yaliyomo ndani ya mapera yanasaidia katika ku-normalise shinikizo la damu ( Blood Pressure )
Ndizi na mapera vina kiwango cha potassium sawa.
6. Utajiri mkubwa wa Madini Ya Shaba
Mapera yana madini ya shaba ( Trace element copper ) ambayo ni mazuri sana katika ku- maintain ufanyaji kazi wa tezi ziitwazo thyroid.
Tezi za thyroid zisipo fanya kazi vizuri zinaweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya kwa mwanadamu.
7. Utajiri wa Madini Ya Manganese
Mapera yana utajiri mkubwa wa madini ya manganese ambayo yanausaidia mwili katika kunyonya ama kupata virutubisho muhimu kutoka kwenye vyakula tunavyo kula.
Chakula tunacho tumia kikitumika vizuri mwilini, tunapata virutubisho vyote muhimu kama vile biotini, vitamin nakadhalika..
8. Kuusadia mwili na akili katika ku-relax
Mapeara yana utajiri mkubwa wa madini ya magnesium ambayo hufanya kazi ya kuvifanya akili na mwili wa mwanadamu viweze ku relax. Unashauriwa kutumia mapera baada ya kazi nzito. Hii itasaidia katika kuufanya mwili na akili yako kupumzika
9. Mapera ni muhimu katika afya ya akili ya mwanadamu.
Vitamin B3, Vitamin B6 ambazo zinapatikana ndani ya tunda la mpera muhimu katika kuimarisha afya ya akili ya mwanadamu.
Mapera yatasaidia kuufanya ubongo wako u relax.
10. NI MUHIMU KATIKA NGOZI YA MWANADAMU.
Vitamin C, viondoa sumu na karotini ambavyo vyote vinapatikana ndani ya tunda la mpera ni muhimu sana katika kuimarisha afya ya ngozi.
Kama hiyo haitoshi, kokwa la mpera huwa linatumika katika kutengeneza vipodozi na losheni kwa ajili ya matumizi ya mwanadamu.
Mapera ni matunda ya msimu yenye wingi wa vitamini A na C, madini ya potasiam, nyuzi nzuri ya fiber na 'lycophene' vyote hivi ni muhimu kwa afya.
Watu wengi hutumia tunda tu pasipokujua si tunda pekee lenye manufaa kwa afya. Majani ya mpera ni mazuri kwa ajili ya ngozi, nywele na afya kwa ujumla. Ifatayo ni njia kadhaa za kutumia majani ya mpera kwa ajili ya afya yako.
FAIDA YA MAJANI YA MAPERA
1. Chai ya majani ya mpera inasaidia mwili kuwa stadi, inasaidia madini ya carbohydrates yasigeuzwe kuwa sukari ndani ya mwili hiyvo kupunguza hamu ya kula.
2. Chai ya majani ya mpera pia inashusha kiwango cha sukari mwilini na kuzuia mwili kuondoa 'insulin'. Kwa sababu ya hii wagonjwa wa sukari wanashauriwa kuitumia mara kwa mara.
3. Chai ya majani ya mpera pia hupunguza lehemu mbaya (bad cholestrol) bila kudhuru lehemu nzuri.
4. Chai hii ina nguvu za kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini hasa kuzuia magonjwa ya kuharisha na kipindupindu.
5. Chai hii inasitisha mchafuko wa tumbo na pia inasaidia kukabili madhara yaletwayo na chakula chenye sumu.
6. Chai hii hutibu kukooa na kupumua kwa tabu.
7. Upatapo uvimbe wa fizi na maumivu mdomoni kama jino kuuma, tafuna majani ya mpera.
8. Kwa matatizo ya homa ya dengue, chemsha glasi mbili na nusu na majani ya mpera (kadiria majani 9) mpaka maji yabakie nusu ya ujazo wa awali.
9. Chai ya majani ya mpera imefahamika kutibu kansa na 'prostrate' kwa wanaume.
10. Chai hii inasaidia kwa wanaume wenye tatizo la kuzalisha (Infertility).
11. Ponda majani ya mpera na kuweka sehemu ya kidonda au iliyokatika kuondoa maambukizi. Kwa maumivu nje ya sikio tumia chai ya majani ya mpera. Tia matone ya chai hii iliyopoa kwenye sehemu iliyoathirika.
13. Majani ya mpera hupondwa na kupakwa eneo lenye muwasho uletwao na allergy.
14. Unapoumwa na wadudu majani yalipondwa ni tiba sahihi.
15. Majani ya mpera yana saidia kupigana na mba na chunusi kutokana na wingi wake wa vitamini C.
16. Kuondoa madoa meusi kwenye ngozi ponda majani ya mpera changanya na maji kiasi na upake badala ya dawa za kawaida.
17. Fanya kama na.16 kwa tatizo la ngozi kuzeeka mapema.
18. Majani ya mpera yanaondoa tatizo la kukatika kwa nywele. Chemsha majani kisha wacha yapoe na ukande kwenye paji na eneo la ngozi taratibu kwa dakika 15. Wacha kwa dakika 30 kisha usha na maji masafi bila shampoo au sabuni. Fanya hivo mara 3 kila wiki.
Wengi waniuliza namna ya kuitengeza chai ya majani wa mpera.
Kuna namna mbili. Aidha chemsha maji kama glasi nne mpaka yachemke sana, chukua majani kama 10 ya mpera, weka ndani ya maji ya moto alafu funika kwa dakika 10 - 15 koroga chuja, chai yako Tayari.
.
Aina ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani yakiwa ndani. Iki-kokota ondoa kwa moto, wacha kwa dakika 10 -15 chuja, chai tayari. Waweza kutumia majani yaliyokauka pia. Kabla sijasahau ni vizuri zaidi ukichanganya na asali badala ya sukari.
Comments
Post a Comment