KISA CHA MWANAFUNZI ROSE
Kuna mwalimu wa shule ya sekondari alikuwa amezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji. Mwanafunzi huyu alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Hivyo, siku ambazo mwalimu huyu alikuwa na kipindi cha kwanza, mwanafunzi huyu alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu. Wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana shuleni. Wiki lililofuata yule mwanafunzi alifika shuleni kabla ya mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alipomwona alifurahi sana. Alipoingia darasani alimwita yule mwanafunzi na kumsifia sana mbele ya darasa. "Rose, simama. Darasa, Mpigieni makofi "Rose" kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Kumbe fimbo zile zimesaidia enhe" Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka huyo "Rose" Yule mwanafunzi alimwomba mwalimu ampe nafasi aseme jambo. Mwalimu akamruhusu "Mwalimu, siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shule nilikuwa namuuguza mama yangu. Baba yang...