KISA CHA MWANAFUNZI ROSE



Kuna mwalimu wa shule ya sekondari alikuwa amezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji. Mwanafunzi huyu alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Hivyo, siku ambazo mwalimu huyu alikuwa na kipindi cha kwanza, mwanafunzi huyu alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu. Wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana shuleni.

Wiki lililofuata yule mwanafunzi alifika shuleni kabla ya mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alipomwona alifurahi sana. Alipoingia darasani alimwita yule mwanafunzi na kumsifia sana mbele ya darasa.

"Rose, simama. Darasa, Mpigieni makofi "Rose" kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Kumbe fimbo zile zimesaidia enhe"

Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka huyo "Rose" Yule mwanafunzi alimwomba mwalimu ampe nafasi aseme jambo. Mwalimu akamruhusu

"Mwalimu, siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shule nilikuwa namuuguza mama yangu. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa. Nimelelewa na mama yangu tu. Simjui ndugu yeyote. Mama yangu alipokumbwa na maradhi alipelekwa hospitalini lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na dawa za kutuliza maumivu tu." Kwa sababu hatuna pesa, hakuweza kupelekwa popote kwa vipimo zaidi."

Rose alifuta machozi yaliyoanza kutiririka mashavuni. Mwalimu jicho nyanya. Rose akaendelea

"Hivyo, nilitakiwa kufanya usafi wa nyumba, kuchota maji, kumsafisha mama yangu, kumwandalia chakula chake kabla ya kuonda kuja shuleni na kazi zingine zote." Rose alinyamaza kidogo."

"Lakini leo nimewahi kwa sababu mama yangu alifariki wiki lililopita. Kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndo maana leo nimewahi shuleni."

Rose hakuweza kuongea tena. Taratibu akakaa kitini huku akilia kwa kwikwi

Darasa zima liligeuka mahala pa msiba.

WITO: Walimu tusiwe tunapenda kuwapa wanafunzi adhabu bila kuwapa nafasi ya kujieleza sababu za kufanya makosa hayo. Wakati mwingine watoto hao huhitaji watu wa kuwasikiliza kwa sababu kwao hawasikilizwi. Ukionyesha upendo huwa inasaidia kuwabadili kitabia mbaya kwenda nzuri...

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI