MKE WANGU SAMAHANI (FULL STORY)
MKE WANGU SAMAHANI
(FULL STORY)
Asubuhi aliamka na kumkuta mkewe akisali. Akamsikia mkewe akimuombea. Akamtazama kwa sekunde kadhaa. Ni muda mrefu sana tokea amemshuhudia mkewe akisali.
Wamekuwa na ugomvi na kutoelewana katika ndoa yao Kwa miezi kadhaa sasa. Usiku wa jana yake wamegombana ugomvi mkubwa mno.
Haraka haraka Mume akainuka kitandani na kuelejea jikoni kuandaa kifungua kinywa. Kwa hio miezi kadhaa ya ugomvi mkewe amekua hamuandalii chakula. Kwa mshangao, akakuta staftahi imeshaandaliwa mezani. Akala.
Baada ya kumaliza akarudi chumbani, kujiandaa aingie bafuni. Mke nae akawa anatoka bafuni. "Habari za asubuhi. Uwe na siku njema". Mke akamsalimia mumewe na kumtakia kazi njema, huku wakipishana bafuni
Baada ya kuoga, na kuvaa tayari kwenda kazini; akamuona mkewe jikoni, akila staftahi akiwa na amani. Alikuwa akila kifungua kinywa huku akicheka kutokana na kuangalia video za vichekesho alizotumiwa WatsApp.
Mume akamtizama kwa dakika kadhaa halafu, akaelekea mlango wa kutokea na kuelekea kazini. Ule mwonekano wa mwisho aliouona kwa mkewe ukamsumbua nafsi.
Akajisemea nafsini mwake.."hivi sivyo inavyotakiwa awe. Hivi sivyo ambavyo amekuwa siku zote." Mume Amekuwa akimuumiza mkewe, na mkewe hivi karibuni amegundua kwamba mumewe anayo nyumba ndogo, na haitoshi amegundua pia anatembea na wanawake wengi.
Amekuwa akitapanya fedha za familia kwa wanawake. Mkewe lazima awe na hasira dhidi yake. Lakini ile amani aliyomuona nayo mkewe asubuhi ile ilimshangaza na kumfanya ajiulize maswali mengi.
Jioni ikafika. Akarudi nyumbani na kukutana na mkewe aliye na amani tele tena. Alikuwa jikoni akipika chakula cha usiku huku akicheka na wanae. Mke alirudi kutoka kazini kama masaa mawili yaliyopita.
Wakala. Chakula kilikua kitamu. Chakula kizuri, mke akawa na maongezi ya furaha na watoto wake baada ya kumaliza kula. Yeye kama baba alikuwa ametengwa kwenye yale maongezi.
Mkewe na watoto wake walionekana kufurahia yale maongezi ingawa baba yao alikuwa akiwaumiza kwa ugomvi na mama yao.
Akiwa anaosha vyombo Baada ya Dinner, huku watoto tayari wakiwa wameshaenda kulala, mume wake akamkaribia. "Uko sawa?" Mume akamuuliza mkewe. "Niko zaidi ya sawa. Nimebarikiwa". Mke akamjibu mumewe huku akitabasamu..
"Umenikasirikia kwa haya nayoyafanya na ambayo nimekufanyia?" Mume akamuuliza tena mkewe.
Mke akaweka kwenye dishi sahani aliyokua anaiosha na kumtazama mumewe. Kisha akaanza kuongea..
"Nilijiuliza nafsi yangu, ni mahusiano gani muhimu katika maisha yangu? Mahusiano niliyonayo na wewe au niliyonayo na Mungu wangu? Na nikagundua mahusiano muhimu kwangu ni yale niliyonayo na Mungu wangu. Naishi kwa ajili ya Mungu. Sio kwa ajili yako...
"Kuolewa na wewe ilikuwa ni baraka lakini si kwamba ndio kila kitu katika maisha. Mungu amenibariki kwa kunipa zawadi ya uhai, sitapoteza uhai wangu kwa kulia kila siku na kuugua vidonda vya tumbo kwa maumivu unayoyasababisha wewe.
Akageukia dishi la vyombo, akachukua bilauri na kuanza kuiosha huku akiendelea kuongea..
"Nimetambua kwamba nilikupa nguvu na uhuru mwingi mno...ndio wewe ni mume wangu, binadamu wa karibu kabisa maishani mwangu na binadamu ninaekupenda sana; lakini wewe sio Mungu. Wewe umefeli lakini Mungu hawezi kufeli na kamwe hawezi kufeli juu yangu..
"Sitaruhusu wewe uniharibie furaha, amani, na maendeleo ambayo Mungu wangu amenipa. Wewe vunja ndoa kama ndio lengo lako, lakini mimi nitaendelea kumtumainia Mungu wangu..na nitakapoendelea kumtumainia Mungu wangu nitazidi kuwa na furaha licha ya kile ambacho utakua umenifanyia.."
Akaisuza vizuri bilauri na kuiweka katika chombo kisafi...kisha akachukua sahani na kuanza kuiosha huku akiendelea kuongea...
"Ulivokua unaniumiza na kunishushia heshima nilikuwa mwanamke nisie na Mungu. Nilikuwa na hasira na kuharakisha matusi, nilikuwa nataka kulipiza kisasi na nilikuruhusu uendelee tu na ufedhuli wako ili na mimi nianze...
"Performance yangu kazini ilishuka, nikawa siongei na wanangu kwa hasira, nikawa mchungu na mkali kwa watoto wangu, nikapata vidonda vya tumbo...ila hatimae nikagundua yupo Mungu, sitakiwi niwe kama mtu ambae hana Mungu..kwanini nisiwe na matumaini wakati Mungu yupo?..
"Nilikuwa nime-focus sana kwako kiasi ya kwamba nikamsahau Mungu. Uliponipata, ulinikuta nikiwa na Mungu. Tukaingia katika mahusiano na hatimae ndoa, nikakuachia kila kitu wewe kwa sababu nilitaka ndoa yangu iwe imara...
"Ndoa yetu ikawa nzuri hapo mwanzoni, ndoa yetu imefeli kwa sababu yako wewe kwa sababu uhusiano wangu na Mungu wangu upo palepale..
Akaisuza vizuri sahani, kisha akamgeukia mumewe..akamtazama na kuendelea kuongea..
"Umechagua kuitelekeza ndoa yetu na kunipa mimi kisogo ila hiyo haimaanishi dunia ndio imenigeukia. Nitaendelea kuwa mama bora kwa watoto wetu. Kamwe hutawasikia wakitamka ugomvi wangu na wako ili nionekane mama niliyefeli..
"Wewe endelea kutembea na hao wanawake zako, mimi nitawalea wanangu...
Akakunja mikono yake kifuani, kisha akaendelea kuongea...
"Je ninakuchukia? Hapana, huo utakuwa uongo kusema nakuchukia. Wewe ni mwanaume niliekubali unioe, ambae niliweka agano mbele za Mungu, ambae nakupenda...
Machozi yakaanza kumtoka....akainua mikono yake kujifuta kisha akaendelea kuongea...
"Siwezi kufuta miaka yote ambayo tumekua pamoja. Biblia hata Quran zinatusisitizia kuwapenda maadui zetu. Ikiwa ninao uwezo wa kuwapenda adui zangu, basi ni rahisi sana kukupenda wewe licha ya mabaya ambayo umenifanyia na unaendelea kunifanyia...
"Ndio ninayo hasira na nilikata tamaa, lakini nimeinuka upya. Naishi kwa ajili ya Mungu ambae amenibariki kwa mengi, sio kwa ajili yako na maumivu unayonipa...
Akageukia vyombo na kuendelea kuosha...kimya kidogo kikapita huku mumewe akiwa ameinamisha kichwa chini.
Mke akavunja ukimya uliokuwa umetawala kwa muda kidogo na kuendelea kuongea...
"Kwa ajili ya amani na kukupa uhuru, nafanya mpango wa sehemu ambayo mimi na watoto tutaenda kuishi. Kwa kuwa umeamua kuwa na nyumba ndogo, uliyoipangia na nyumba kabisa, imeonesha kabisa sisi hautuhitaji...
"Hivyo hatutafanya maisha yako yawe ya wasiwasi na kutokuwa comfortable kwa kuendelea kukulazimisha kuishi na sisi...unatakiwa uwe huru kumleta huyo mchepuko wako ndani ya nyumba yako mwenyewe wala sio kumpangia nyumba...
"Nilikuja kwa amani ndani ya hii nyumba, na nitaondoka kwa amani. Hautaua tabasamu na furaha yangu...Mungu wangu hataniangusha katika hili..."
Mke akamaliza na akaelekea chumbani. Mume akabaki pale kama nusu saa akitafakari na baadae mume akamfuata mkewe chumbani. Akamkuta mkewe akiwa amelala kwa amani zote. Akamtikisa na kumuamsha. Mkewe akaamka..
"Nakusikiliza...ongea tu" mke akamwambia mumewe...
"Tafadhali sana mke wangu, msiondoke! Sitakuumiza tena, sitakusaliti tena. Kusema kweli mimi siko sawa kabisa. Nahitaji hiyo amani uliyonayo. Nahitaji kuwa aina ya mume kama wewe ulivyo aina ya mke..ili tuweze kuendana...
"Nimejikuta naumia zaidi kukutenda mabaya, lakini wewe ukiwa bado na amani na furaha tele..hicho kitu kinaniumiza ndani kwa ndani. Namimi nimeamua kurudi kwako...nipokee tena mpenzi wangu..."
Kuanzia siku hiyo, mume akaanza kubadilika huku mkewe akimsaidia kubadilika..hakukuwa na michepuko, hakukuwa na ugomvi, wala kumuumiza tena mkewe...
Mkewe na wanae hawakuondoka. Mume akajinyenyekeza kwa Mungu na akajifunza kuwa mume na baba bora.
Upendo una nguvu kubwa kiasi ya kupunguza kila aina ya ufedhuli.
_____________________________
Sijajua bado ni suala gani gumu unalolipitia mpaka siku hii..ni maombi yangu kwako Mungu akuvushe katika kila aina ya gumu unalopitia..na tazama mvua ya amani itaenda kukunyeshea ikileta uhuru na kumwagilia mbegu ya baraka katika maisha yako.
A M E N

Comments
Post a Comment