FAHAMU JINSI YA KUTENGENEZA SCRUB



FAHAMU JINSI YA KUTENGENEZA SCRUB

Habari zenu wapendwa.

Leo nimewaletea somo la utengenezaji scrub ukiwa nyumbani kwako na kwa mahitaji rahisi Sana yanayopatikana nyumbani kwako.



Mahitaji

Sukari nyeupe kikombe kimoja
Asali kijiko kimoja cha chakula
Ndimu mbili
Unga wa majani ya chungwa kijiko kimoja cha chakula
Mafuta ya mzeituni kijiko kimoja cha chakula

Namna ya kutengeneza.

Chukua bakuli lako anza kuweka Sukari..asali..ikifuatiwa na maji ya ndimu Kisha changanya na kijiko.
Baada ya hapo weka unga wako wa majani ya chungwa,Kisha weka mafuta ya mzeituni..changanya vizuri hakikisha mchanganyiko wako unachanganyika vizuri.

Faida za utumiaji scrub hii ni hizi zifuatazo;

Kuvua gamba au kuondoa ngozi ya juu iliyokufa.

Kufanya ngozi kuwa laini.

Kuipa ngozi yako mn'gao.

Kurudisha ngozi katika uhalisia wake hasa ngozi iliyoungua na jua.

Kuondoa makunyazi ya mwilini.

Kuondoa mabaka mwilini.

Sio lazima utumie maji ya ndimu waweza tumia lemon essential oil 10drops.

Scrub hii inadumu kwa muda wa week mbili Kama utatumia ndimu na kuweka kwenye friji na ukitaka idumu hata mwezi hakikisha wakati wakati wa kuichota hautumii mkono tumia kijiko kwenye uchotaji wa scrub yako.

Nimemaliza ..Ahsanteni.

Alamsik.

Post nyingine bora kwa ajili yako


  1. Magonjwa hatari na afya

  2. Hadithi tamu na za kusisimua

  3. Mkala maalumu za dini

  4. Jifunze kutoa huduma ya kwanza

  5. Makala za sayansi na teknolojia

  6. Masomo ya Shule na mitihani

  7. Chemsahabongo

  8. Faida za mboga na Matunda

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI