UMUHIMU WA KOKOTO KUTANDAZWA KWENYE RELI
Kusafiri ndani ya treni (garimoshi) kuna upekee wake.
-
Moja ya kitu cha pekee utakachokiona ni mawe madogo madogo(kokoto) kuzunguka reli ambapo treni inapita.
-
Lakini umewahi kujiuliza kwanini reli imetandazwa kokoto hizo?
1- Mawe ya relini yanafanya kazi nyingi. Kwanza kabisa, yanasaidia reli kukaa mahali pake wakati treni yenye uzito mkubwa ikiwa inapita
-
2- Pia yanazuia aina yoyote ya majani yasiote karibu na reli ambayo yanaweza kuufanya udongo uliopo chini ya reli kuwa dhaifu na kushindwa kuhimili uzito wa reli na treni
-
3- Kazi nyingine muhimu inayofanywa na mawe ya relini ni kuzuia maji yasikusanyike au kukaa muda mrefu kwenye reli na kudhoofisha njia ya reli
-
Hivyo basi ni jukumu letu sote kulinda na kuhakikisha mawe hayo hayaondolewi kwenye reli kwasababu yamewekwa kwasababu maalumu ya kuimarisha reli na kuwalinda watu wanaotumia usafiri wa treni...
Comments
Post a Comment