VYAKULA VITAKAVYOKUONGEZEA KINGA YA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA CORONA ( COVID-19)
VYAKULA VITAKAVYOKUONGEZEA KINGA YA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA CORONA ( COVID-19)
Njia za kufuata ili kuimarisha kinga ya mwili ili kupambana na maambukizi ya virusi vya corona
Kwa kutambua umuhimu wa kuchukua tahadhari ya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona, nimeamua kutumia jukwaaa hili kufafanua mambo machache kuhusu kinga ya mwili (body immunity) na makundi machache ya vyakula vinavyopatikana kwa urahisi ambavyo vinauwezo wa kuongeza na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili( body immune system). Twende pamoja;
1. Hiriki
Mbali na kiungo hiki kutumika kuongeza radha katika vyakula na vinywaji, hiriki ni chanzo kizuri cha madini muhimu mwilini. Madini haya ni kama vile potassium, calcium, madini ya chuma na manganese. Madini haya husaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mapafu na kuzibua mirija ya hewa, hivyo kuwapa unafuu watu wenye matatizo ya pumu na kupumua.
Pia hiriki ina vitamini mbali mbali kama vile vitamin A, B na C ambavyo husaidia kuimarisha kinga ya miili yetu.
2. Matunda jamii ya machungwa na malimao
Matunda jamii ya machungwa yana kiwango kikubwa cha vitamin C na virutubisho vya flavonoids ambavyo husaidia kupunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo. Vitamin C vinavyopatikana kwenye chungwa pamoja na vitamin B-6 na madini ya chuma, ni virutubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oxygen mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu na matatizo ya kupumua.
Vile vile, vitamin C vilivyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe za damu (WBC's) ambazo ni muhimu kwa uimarrishaji wa kinga ya mwili.
Matunda mengine ni papai, pera na parachichi.
3. Tangawizi (ginger)
Husaidia kupunguza lehemu katika mishipa ya damu na kuzuia damu kuganda katika mishipa, hivyo kuzuia madhara ya kuziba kwa mishipa ya damu jambo ambalo lisipodhibitiwa linaweza kusababisha maradhi ya moyo na kupooza kwa viungo vya mwili. Vile vile, tangawizi husaidia kutibu kuwashwa na kukereketwa koo(sore throat) na kuondoa kabisa mafua au flu.
4. Supu ya kuku
Ulaji wa supu ya kuku wa kienyeji husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu (WBC's) ambazo husaidia kuimarisha kinga ya mwili. Pia supu ya kuku husaidia kupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa (respiratory system).
5. Samaki
Samaki ana madini ya zinc ambayo hupatikana kwenye seli zote za mwili. Madini haya husaidia kinga ya mwili kufanya kazi yake kwa ufanisi. Kumbuka, kiasi kingi cha madini ya zinc huathiri utendaji kazi wa kinga ya mwili hivyo inashauriwa kutumia milligram 11 kwa mwanaume mtu mzima na milligram 8 kwa mwanamke kwa kila mlo wa siku.
6. Broccoli
Broccoli ni mboga jamii ya cruciferous ambayo hupatikana kwenye mimea aina ya brassica. Broccoli ina madini ya zinc ambayo husaidia kinga ya mwili kuwa imara na kufanya kazi yake kwa ufanisi. Kumbuka; mboga yoyote ya majani inatakiwa kuchemshwa kiasi ili kuepuka kupoteza virutubisho muhimu.
7. Spinachi
Ni mboga ya majani, faida yake mwilini haina tofauti sana na broccoli. Pia ina beta-carotene ambayo husaidia kuimarisha afya ya ngozi na macho.
8. Mbegu za alizeti na maboga
Mbegu hizi zina madini ya zinc ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili.
9. Mtindi(yogurt)
Maziwa yanayotokana na ng'ombe. Maziwa haya ni chanzo kikubwa cha vitamin D ambavyo husaidia kuongeza kinga ya asili ya miili yetu dhidi ya magonjwa.
10. Maji
Maji ndio uhai wenyewe. ili kinga yako ifanye kazi inategemea sana uwepo wa maji mwilini, hivyo ili kuongeza kinga ya mwili hakikisha unakunywa maji ya kutosha kulingana na uzito wako hasa kabla ya kula kitu chochote.
Mbali na vyakula, mambo mengine ambayo yanaweza kuimarisha kinga ya mwili wako ni pamoja na;
1. Kupata usingizi wa kutosha
2. Kupunguza msongo wa mawazo (stress)
3. Kunywa kiasi kidogo cha pombe (kwa watumiaji wa pombe)
4. Kuepuka uvutaji wa sigara
5. Kufanya mazoezi ya mwili (physical exercise).
Kumbuka: suala la kuimarisha na kuongeza kinga ya mwili linapaswa kuwa suala endelevu la kila siku kwa mustakabali wa afya yako.
Comments
Post a Comment