KISA CHA MFUGAJI NA FARASI WAKE.



Mfugaji mmoja alikuwa anafuga farasi na kondoo, alimtumia farasi kwa usafiri wake.
 Siku moja farasi wake aliugua akaamua kumtafuta daktari wa mifugo amtibu haraka. Daktari wa mifugo akajaribu kumpatia dawa, akamwambia mfugaji kuwa ile dawa lazima iwe imemtibu farasi ndani ya siku 5 na kama zitafikia siku 5 hajapona basi itabidi achinjwe maana ni ishara tosha kuwa hatapona tena sababu ya mashambulizi makubwa ya bakteria. Daktari Akaondoka kwa ahadi ya kurudi tena kuangalia maendeleo ya farasi.

 Kondoo alikuwa pembeni akisikiliza kwa makini mazungumzo yao.
 Siku ya pili ilipofika, kondoo akamfuata farasi akamwambia "jitie nguvu rafiki yangu amka kama sivyo watakuchinja."
Lakini farasi hakuwa na nguvu, alishindwa kabisa kuamka.
Ikafika siku ya tatu, kondoo akarudia tena kumwambia : "Amka rafiki. yangu, sitaki kuona unachinjwa, jikaze na mimi nitakusaidia kukushika usianguke, haya twende! Moja mbili tatu….." Jitihada za kondoo zikawa bure maana farasi hakuweza hata kusogea.

Ilipofika siku ya nne daktari akaja kumuangalia tena farasi, akasema kwa bahati mbaya bakteria wamekomaa sana hivyo uwezekano wa farasi kupona haupo, itabidi kesho farasi achinjwe.
 Mfugaji akakubali akaanda vifaa vyote vya machinjio. Kondoo akaumia sana kujua kuwa kesho ndio siku ya mwisho ya rafiki yake farasi, akadhamiria kumsaidia kwa gharama yoyote ile ili asichinjwe.
 Ilipofika asubuhi ya siku maalumu kondoo akamfuata farasi kwa huzuni akasema: "sikiliza rafiki yangu, wakati wa kujaribu ni sasa au hutakaa ujaribu kamwe maana hutakuwa na nafasi nyingine ukishachinjwa.

 Akaanza kumtia moyo kwa maneno ya matumaini "Amka, simama, kaza miguu, Kuwa na ujasiri, polepole tembea, tembea rafiki, Haya njoo, moja , mbili, tatu... Good, vizuri. Sasa kwa kasi tembea..tembea.. endelea kutembea ..." Kondoo akazidi kumtia moyo farasi, " Haya kimbia, kimbia zaidi! Ndiyo! Yeah! Ndiyo! Unaweza, wewe ni bingwa!!!!!"... Kondoo akazidi kumtia moyo farasi, Kwa mbinu alizompa na maneno yale ya kutia moyo ya kondoo yule farasi akapata nguvu akaanza kukimbia.

Ghafla mfugaji akatokea, akamwona farasi wake anapiga mbio uwanjani huku pembeni yupo kondoo, mfugaji akafurahi sana kupita kiasi, akaanza kupiga kelele: "Jamani njooni muone muujiza! farasi wangu kapona. Anakimbia jamani!!, alikuwa hawezi hata kusimama, njooni muone Leo anakimbia! Lazima nifanye sherehe kubwa! haraka sana mchinjeni kondoo tule tusherekee!!! Watu wote njoonii!!!!!"..Majirani wakajumuika kushiriki furaha ya mwenzao, kondoo akakamatwa akachinjwa, sherehe kubwa ikafanyika.... Huo ukawa mwisho wa kondoo. Maskini Kondoo!!

FUNDISHO:
Kuna watu huchangia sana mafanikio ya watu wengine, lakini mwisho wa siku hawa watu hawatambuliki wala mchango wao huwa hauonekani katika jamii. Sifa na pongezi zinamuendea mtu mwingine bila kujua kuwa kuna mtu nyuma ya pazia aliumia na kutumia gharama nyingi katika kumsapoti huyu anayeoneka leo kuwa amefanikiwa.

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI