KIAFYA: HAISHAURIWI KUFANYA YAFUATAYO BAADA YA KULA CHAKULA:
1.Kuvuta sigara
Kiafya mara baada ya kula chakula hairuhusiwi kuvuta sigara japo kuwa mvutaji wa siagara hupatwa na hamu kubwa ya kuvuta mara baada ya kula tabia hii huhatarisha afya, hivyo inashauriwa kusubiri angalau kwa masaa kadhaa ndipo uvute endapo ni lazima sana kwani sigara ina miliki Nikotini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, madhara yanayotokea kwa kuvuta sigara mara baada ya kula chakula ni sawa na madhara yanayotokea kwa mtu aliyevuta sigara 10 kwa mara moja na hii huchangia mtu kupata kansa ya mapafu.
2. Kula matunda
Wanasayansi wamedhihirisha kuwa kiafya matunda yanatakiwa kuliwa kabla ya kula si mara baada ya kula kama ambavyo imezoeleka kwa watu wengi, Matunda yana enzymes na asali asili ambayo inahitaji kumeng’enywa ndani ya muda wa kutosha, hivyo kula matunda baada ya chakula inaweza kusababisha matatizo ya mmeng’enyo wa chakula pamoja na kiungulia.
3. Kulala
Kulala mara baada ya kula ni kitendo ambacho hupendelewa kufanywa na mamilioni ya watu japokuwa tabia hii si nzuri kiafya, kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wansayansi wa chuo kikuu cha Loannina Medical watu wanaosubiri kulala kwa kitambo kidogo mara baada ya kula wana nafasi ndogo ya kupata ugonjwa wa mshtuko na hii ndio sababu inashauriwa kukaa masaa mawili mara baada ya kula ndipo kulala.
4. Kuoga
Kuoga mara baada ya kula ni moja ya kitu kibaya na hatari sana kwani kwa kufanya hivyo unaweza kudhuru afya yako, Kuoga maji ya moto kunasababisha kuongeza kasi ya mzunguko wa damu kwenye miguu na kupunguza kasi ya mzunguko wa damu tumboni kitu ambacho kina madhara kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
5. Kunywa Chai
Chai humiliki asidi aina ya Tannic ambayo inakusanya pamoja madini ya chuma na protini kwenye chakula, matokeo yake ni kwamba 87% ya madini ya chuma hupungua kwa kiasi kikubwa hali inayopelekea mtu kukumbwa na magonjwa kama Anemia, kizunguzungu na kuchoka kutokana na kukosa madini ya chua mwilini.
Comments
Post a Comment