JE! NINI HUSABABISHA WANAWAKE VIUNO VYAO KUUMA??
Maumivu ya kiuno kwa wanawake huwa yana sababu nyingi. Mengine yanahusiana na hali maalumu kwa wanawake, huku mengine yanaweza kujitokeza tu kwa mtu yeyote. Katika makala hii tutaangalia visababishi vya maumivu ya kiuno kwa wanawake, hivyo kila mmoja mwenye tatizo hili ataona umuhimu wa kwenda kupima na kuweza kupata matibabu. Je, Nini Husababisha Kiuno Kuuma? Baadhi ya visababishi vya maumivu ya kiuno kwa wanawake hutokana na hali maalumu, nazo zipo kama ifuatavyo; 1. Ugonjwa Wa Kabla Ya Hedhi(PMS) Hii huwa ni hali ambayo wanawake wengi huipata kabla ya vipindi vyao vya hedhi. Hali hii ina dalili nyingi, lakini hutaziona zote. Kwa kawaida dalili hizi huwa kama hivi; a) Dalili Za Mwili, kama vile; •Maumivu ya kiuno • Kichwa kugonga • Uchovu • Tumbo kuunguruma b) Dalili Za Kihisia Na Kitabia, kama vile; • Kubadilika badilika kwa hali ya moyo • Kutamani vyakula • Wasiwasi • Shida kuzingatia • Kujikita kwenye tatizo Ugonjwa wa kabla ya hedhi(Premenstrual Syndrome au PMS) huanza siku chach...