KWANINI UTI INAWASUMBUA SANA WANAWAKE KULIKO WANAUME??

 




KWA NINI UTI INAWASUMBUA WANAWAKE ZAIDI KULIKO WANAUME?


UTI (Urinary tract infection) ni ugonjwa wa maabukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya yanasababishwa na bakteria aitwaye Escherichia coli.  

Kwa kawaida bakteria hawa hupatikana katika utumbo mpana na kwenye njia ya haja kubwa na inapotokea wakahamia katika njia ya mkojo husababisha mtu kupata tatizo hili la maambukizi katika mfumo wa mkojo. Ugonjwa wa U.T.I unaweza athiri urethra, kibofu cha mkojo na figo.


DALILI ZA UTI

➢ Kwenda haja ndogo mara kwa mara na maumivu wakati wa kukojoa

➢ Kuhisi kuunguzwa na mkojo kwenye kibofu au mrija wa mkojo

➢ Maumivu chini ya kitovu.

➢ Mkojo kuwa na harufu mbaya na pia kubadilika rangi kuwa nyeusi au rangi ya mawingu.

➢ Kuhisi homa kali na uchovu na kichefuchefu.

➢ Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo.

➢ Maumivu ya mgongo na kiuno. 

➢ Uchovu kupita kiasi wa mwili mzima. 

➢ Kupata hamu kubwa ya kwenda haja ndogo lakini inatoka kiduchu. 

➢ Haja ndogo kutoka legevu au legelege.


KWANINI WANAWAKE NDO WAHANGA WAKUBWA?

Wanawake ni wahanga wakubwa sana wa ugonjwa huu kulingana na maumbile yao yalivyo kwa kuwa njia ya mkojo na njia ya haja kubwa zipo karibu hivyo ni rahisi bakteria hawa kuhama kutoka njia ya haja kubwa kuja njia ya haja njogo.

Pia Urethra (mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu) kwa wanawake ni mfupi sana hivyo kuruhusu bakteria kufika kwa haraka kwenye kibofu.

Wanawake wengi huwahamisha bakteria hawa kwa njia ya kujisafisha baada ya kujisaidia, kwani hujisafisha kutoka nyuma kuja mbele badala ya kujisafisha kutoka mbele kwenda nyuma na hutakuwi kurudi tena mbele.


Ugonjwa huu usipotibiwa unaweza kuathithiri figo na kufanya matibabu yake yawe na gharama kubwa pia na kugharimu maisha. Ni vema kuzingatia usafi wa mwili na mavazi unywaji wa maji mengi na kufuata ushauri wa kitaalamu ili kuboresha afya zetu.


🤝🙏🥗🍲🍵

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI

ZIJUE FAIDA KUMI (10) ZA STRAWBERRY MWILINI