JE! NINI HUSABABISHA WANAWAKE VIUNO VYAO KUUMA??



Maumivu ya kiuno kwa wanawake huwa yana sababu nyingi. Mengine yanahusiana na hali maalumu kwa wanawake, huku mengine yanaweza kujitokeza tu kwa mtu yeyote. Katika makala hii tutaangalia visababishi vya maumivu ya kiuno kwa wanawake, hivyo kila mmoja mwenye tatizo hili ataona umuhimu wa kwenda kupima na kuweza kupata matibabu.

Je, Nini Husababisha Kiuno Kuuma?


Baadhi ya visababishi vya maumivu ya kiuno kwa wanawake hutokana na hali maalumu, nazo zipo kama ifuatavyo;


1. Ugonjwa Wa Kabla Ya Hedhi(PMS)

Hii huwa ni hali ambayo wanawake wengi huipata kabla ya vipindi vyao vya hedhi. Hali hii ina dalili nyingi, lakini hutaziona zote. Kwa kawaida dalili hizi huwa kama hivi;


a) Dalili Za Mwili, kama vile;

•Maumivu ya kiuno

• Kichwa kugonga

• Uchovu

• Tumbo kuunguruma


b) Dalili Za Kihisia Na Kitabia, kama vile;

• Kubadilika badilika kwa hali ya moyo

• Kutamani vyakula

• Wasiwasi

• Shida kuzingatia

• Kujikita kwenye tatizo


Ugonjwa wa kabla ya hedhi(Premenstrual Syndrome au PMS) huanza siku chache kabla ya kipindi cha hedhi, na huisha ndani ya siku moja au mbili baada ya kipindi cha hedhi kuanza. 


2. Endometriosis

Endometriosis ni ugonjwa ambapo tishu laini inayokuwa kwenye ukuta wa ndani ya tumbo la uzazi, kitaalamu hufahamika kama, “endometrial tissue”, huota nje ya tumbo la uzazi. 

Tishu hii mara nyingi huota kwenye vifuko vya mayai, mirija ya uzazi, pamoja na tishu zingine zinazotanda kwenye nyonga. Inaweza pia kuota kwenye mrija wa mkojo na njia ya haja kubwa.

NUKUU: Maumivu huwa ni dalili ya kawaida katika ugonjwa wa endometriosis. Dalili zingine ni pamoja na;


• Maumivu makali sana wakati wa hedhi

• Maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa

• Maumivu ya kiuno au nyonga

• Maumivu wakati wa kujisaidia nhaja kubwa 

• Maumivu wakati wa kukojoa hasa unapokuwa hedhini


Endometriosis inaweza pia kusababisha kutokwa na damu mara mbili ndani ya mwezi mmoja. Matatizo ya tumbo kama vile kuharisha au tumbo kuunguruma yanaweza kuwa ya kawaida pia, hasa wakati wa hedhi. Endometriosis inaweza kukufanya mwanamke usipate ujauzito kwa urahisi.


3. Maumivu Makali Wakati Wa Hedhi

Kipindi cha hedhi chenye maumivu makali kitaalamu tunaita, “Dysmenorrhea”. Ingawa kwa kawaida hali hii huwa inavumilika, lakini bado maumivu huwa ni makali mno kwa baadhi ya wanawake.


NUKUU: Unaweza kuwa katika vihatarishi vikubwa vya maumivu makali yahedhi ikiwa kama wewe;


• Uko chini ya umri wa miaka 20

• Ni mvuta sigara

• Unatokwa na damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi

• Una magonjwa kama hayo hapo chini kama vile;


I. Uvimbe wa fibroid kwenye mfuko wa uzazi

II. Maambukizi katika via vya uzazi


NUKUU: Maumivu yatokanayo na hedhi mara nyingi husikika maeneo ya tumbo la chini, kiunoni, hips, na miguuni. Mara nyingi maumivu haya huchukua muda wa siku 1-3. Maumivu yanaweza kuwa ya makali na yenye kuchomachoma au yanaweza kusikika katika hali ya mshituko fulani.


4. Ujauzito

Maumivu ya mgongo huwa ni yakawaida wakati wa ujauzito. Hutokea pale kituo chako cha mvuto kinapohama, unapopata uzito mkubwa, na homoni zako ili kujiandaa kwa ajili ya kuzaa.  Wanawake wengi hali ya maumivu ya kiuno hutokea kati ya mwezi wa tano au saba wa ujauzito, lakini tatizo hilo linaweza kuanza mapema. Unaweza kupatwa na hali hiyo wakati wa ujauzito ikiwa kama tayari una matatizo ya kiuno.

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI