ZUJUE SABABU ZA TUMBO KUJAA GESI



Chakula kutokusagwa au mchafuko wa tumbo ni msemo wa kawaida ambao huelezea masumbufu ndani ya tumbo lako la juu. Chakula kutokusagwa sio ugonjwa, bali kuna baadhi ya dalili unaweza kuzipata, ikiwa pamoja na maumivu ya tumbo na kujisikia tumbo kujaa gesi muda mfupi tu unapoanza kula. Ingawa hali ya tumbo kujaa gesi huwa ni ya kawaida, lakini kila mtu anaweza kupatwa na hali ya kukosa choo katika njia tofauti. Dalili za tumbo kujaa gesi unaweza kuzihisi mara kwa mara au kila siku.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?


Watu wenye tatizo la tumbo kujaa gesi kwa karne hii ni wengi sana, na dalili zake huwa kama hivi ifuatavyo;

• Tumbo kujaa haraka tu wakati unapokula hata kama ni chakula kidogo

• Kutokujisikia vizuri baada ya kumaliza kula

• Kuhisi masumbufu kwenye tumbo la chakula

• Kuhisi kama hali ya kuwaka moto maeneo ya tumbo la juu

• Tumbo kuunguruma

• Kuhisi kichefuchefu


NUKUU: Wakati mwingine watu wenye tatizo hili pia huhisi kiungulia, lakini kiungulia na tumbo kujaa gesi ni hali mbili zinazotofautiana. Kiungulia ni maumivu au kuhisi kuwaka moto maeneo ya katikati ya kifua chako ambayo yanaweza kupenya shingoni mwako au mgongoni wakati au baada ya kumaliza kula.


Je, Unapaswa Kufanya Nini Inapotokea Hali Hii?


Inapotokea hali ya kawaida tu ya tumbo kujaa gesi hupaswi kubabaika sana. Fika hospitali ikiwa kama masumbufu yanaendelea zaidi ya wiki mbili. Onana na daktari haraka kama maumivu ni makali au kama yanaambatana na:

• Mwili kupungua uzito au kutokuwa na hamu ya kula chakula

• Kurudia kutapika au kutapika damu

• Kutoa kinyesi cheusi

• Kushindwa kumeza chakula

• Mwili kuchoka au kudhoofika, hali ambayo huashiria kupungukiwa damu

Tafuta haraka tahadhari ya matibabu endapo kama utahisi hali mbaya zaidi kama hizi zifuatazo;

• Kukosa pumuzi,

• Kifua kuuma au kuwa na msongo wa mawazo.

• Kutokwa na jasho jingi au maumivu ya kifua yakipenya mpaka kwenye taya, shingo au mkono

Je, Nini Visababishi Vyake?


Hali ya tumbo kujaa gesi ina visababishi vingi. Mara nyingi, tumbo kujaa gesi linahusika na mitindo ya maisha ya wanadamu na inaweza kusababishwa na ulaji wa vyakula vibaya, vinywaji vibaya au utumiaji wa madawa mabaya. Vyanzo vya kawaida vya tumbo kujaa gesi ni pamoja na:

• Kula kupita kiasi au kula haraka haraka

• Kula vyakula vyenye mafuta mengi au vyenye vikolezo vingi

• Unywaji wa kahawa sana, au pombe nyingi, au vinywaji vyenye chokoleti

• Uvutaji sigara

• Msongo wa mawazo

• Matumizi ya madawa ya kutuliza maumivu kama vile panado, diclopa, nk


Wakati mwingine tumbo kujaa gesi husababihwa na hali zingine za umeng’enyaji chakula tumboni ikiwa pamoja na;


• Tumbo kuvimba

• Vidonda vya tumbo

• Mawe ya nyongo

• Kukosa choo

• Saratani ya tumbo la chakula

• Utumbo kuziba

• Kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye utumbo

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI