KISA CHA MFUGAJI NA FARASI WAKE.
Mfugaji mmoja alikuwa anafuga farasi na kondoo, alimtumia farasi kwa usafiri wake. Siku moja farasi wake aliugua akaamua kumtafuta daktari wa mifugo amtibu haraka. Daktari wa mifugo akajaribu kumpatia dawa, akamwambia mfugaji kuwa ile dawa lazima iwe imemtibu farasi ndani ya siku 5 na kama zitafikia siku 5 hajapona basi itabidi achinjwe maana ni ishara tosha kuwa hatapona tena sababu ya mashambulizi makubwa ya bakteria. Daktari Akaondoka kwa ahadi ya kurudi tena kuangalia maendeleo ya farasi. Kondoo alikuwa pembeni akisikiliza kwa makini mazungumzo yao. Siku ya pili ilipofika, kondoo akamfuata farasi akamwambia "jitie nguvu rafiki yangu amka kama sivyo watakuchinja." Lakini farasi hakuwa na nguvu, alishindwa kabisa kuamka. Ikafika siku ya tatu, kondoo akarudia tena kumwambia : "Amka rafiki. yangu, sitaki kuona unachinjwa, jikaze na mimi nitakusaidia kukushika usianguke, haya twende! Moja mbili tatu….." Jitihada za kondoo zikawa bure maana farasi hakuwez...