FAHAMU YA KWAMBA MBEGU ZA MPAPAI



Ndugu yangu msomaji fahamu ya kwamba mbegu za mpapai zinatibu magonjwa mengi kwa mtu mwenye kujua kuzitumia.


NAMNA YA KUZIANDAA:-

Utazichukua mbegu za mpapai utazianika ndani mpaka zikauke hakikisha zisipatwe na mwanga wa jua, zikikauka utazitwanga kisha utazichekesha unga wake utauhifadhi kwa ajili ya kutumia,utatumia kwa maradhi haya yafuatayo:-


TIBA YA KISUKARI:-

Utakoroga uji mwepesi kikombe kimoja kisha utaweka unga wa mbegu za papai vijiko viwili vya chakula utakua unakunywa asubuhi na jioni kikombe kimoja asubuhi kingine jioni utaendelea na tiba hii hata kwa muda wa wiki mbili mpaka utaona mabadiliko.hii ni Tiba nzuri sana.

TIBA YA KIDONDA:

Ikiwa mtu anakidonda katika mwili wake anatakiwa akioshe kisha anyunyizie unga wa mbegu za mpapai asubuhi na jioni kitapona haraka.

TIBIA YA KIKOHOZI

Ikiwa mtu ana kohoa basi achukuwe kijiko kidogo cha unga wa mbegu za papai awe anabwiya asubuhi na jioni kwa muda wa wiki au achukuwe kijiko kimoja atie kwenye kikombe cha maji ya moto akoroge anywe asubuhi na jioni kwa muda wa siku tatu.

TIBA YA PUMU:-

Ikiwa mtu ana pumu achukuwe kijiko kikubwa cha mbegu za unga wa mpapai atie kwenye maji ya moto anywe asubuhi na jioni kwa muda wa wiki.


TIBA YA PRESHA:

Ikiwa mtu ana presha basi kila siku asubuhi na mchana na jioni apate kijiko kimoja cha unga wa mbegu za mpapai atie kwenye glasi moja ya maji ya moto anywe.

TIBA YA MTOTO MWENYE MARADHI YA MARA KWA MARA:-

Mpe kijiko kimoja cha unga wa mbegu za papai kisha mkorogee kwenye maziwa glasi moja asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja au mpaka siku kumi atapona biidhni Allah.

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI

ZIJUE FAIDA KUMI (10) ZA STRAWBERRY MWILINI