UJUE UGONJWA WA FIGO(KIDNEY FAILURE)
Figo ni moja ya kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu na hufanya kazi za kudhibiti na kuhifadhi virutubishi na maji na kuondoa mabaki kupitia mkojo*
*Pia figo husaidia sana kuchuja damu ili kuondoa mabaki ambayo ni sumu mwilini. Baadhi ya mabaki hayo ni urea, uric acid, creatinine na ammonia*
*Sababu zinazoweza kufanya figo zishindwe kufanya kazi*
*Sababu za muda mfupi*;
*1️⃣Matumizi ya baadhi ya dawa za kupunguza maumivu*
*2️⃣Upungufu mkubwa wa ujazo wa damu (kupoteza damu kwa kiasi kikubwa)*
*3️⃣Upungufu wa maji mwilini kutokana na kutapika, kuhara, na homa*
*4️⃣Maambukizi kwenye figo mfano sepsis*
*5️⃣Uvimbe mkubwa wa tezi dume (prostatic hypertrophy)*
*Sababu za Muda Mrefu*
*1️⃣Maambukizi katika njia ya mkojo ya mda mrefu(UTI SUGU)*
*2️⃣Kisukari kisichodhibitiwa*
*3️⃣Shinikizo kubwa la damu lisilodhibitiwa*
*4️⃣Uvimbe-uchungu wa kudumu kwenye mfumo wa uchujaji wa figo(chronic glomerulonephritis)*
*5️⃣Mawe kwenye figo*
6️⃣Magonjwa ya tezi dDAMU
(Prostate disease)
*CHANGAMOTO za UGONJWA wa FIGO*;
~FIGO ni OGANI inayoshirikiana na MOYO KUATHIRIKA kwake kuna ATHARI KUBWA kwa MFUMO wa DAMU na MAPIGO ya MOYO,
MAGONJWA SUGU ya FIGO hutokea pale OGANI hiyo inapopoteza UWEZO wa kutenda KAZI zake kikamilifu.TATIZO huanza TARATIBU na KUDUMU kwa MUDA mrefu hadi kuonyesha DALILI za WAZI.
HUU ni kati ya MAGONJWA yasiyoambukiza kwani UNATOKANA na MIENENDO na MITINDO ya KIMAISHA
-FIGO huwa na KAZI ya kuchuja TAKAMWILI zilizo NDANI MWILINI na kuzitoa NJE kwa NJIA ya MKOJO na KUPUNGUZA kiasi cha MAJI kilichozidi MWILINI
-FIGO hutoa HOMONI inayochochea OGANI zingine MWILINI ikiwamo KUHAMASISHA utengenezwaji wa CHEMBE NYEKUNDU za DAMU,utendaji wa MADINI ya Calcium na HOMONI zinazoongeza MWENDO KASI wa MISULI ya MOYO
-Vilevile FIGO hufanya KAZI ya KUFYONZA na KUVIRUDISHA vitu MUHIMU ambavyo vingehitajika kutoka kwa NJIA ya MKOJO
-Hudhibiti MADINI kama POTACIUM,MAGNESIUM,na TINDIKALI ili kuweka sawa MAZINGIRA sawia katika DAMU
Comments
Post a Comment