TATIZO LA MIGUU KUVIMBA NA KUWAKA MOTO


 


Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto Na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili yaani miguu na mikono. 


Tatizo hilo kitaalamu hujulikana kama Peripheral Neuropathy. 

Matatizo haya kiafya miguu au mikono kuhisi ganzi,baridi au maumivu husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguu au mikono) na hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguu au mikono. 


Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo:- 

01. Mtu kuhisi ganzi 


02. Kushindwa kushuka au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli, n.k 


03. Maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguu/mikono. 


Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi ni vizuri nazo ukajua. 


1. Kupungua kwa virutubisho miwilini, hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex) 


2. Matumiz ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu, au dawa za kupambana na virusi vya ukimwi (HIV)


3. Uzito mkubwa wa mwili 


4. Ugonjwa wa kisukari (diabetes poly neuropathy)


5. Shinikizo la damu (pressure)

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI