TATIZO LA MIGUU AU MIKONO KUUMA/KUFA GANZI
Matatizo ya miguu/mikono kuhisi ganzi au maumivu husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa Neva za pembezoni mwa mwili (peripheral neuropathy), hivyo kusababisha kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika eneo husika (miguuni au mikononi).
DALILI ZA TATIZO
>>Mtu kuhisi miguu/mikono kufa ganzi
>>Maumivu au kuhisi kama vile moto unawaka miguuni au mikononi
>>Kuhisi kama vile umevaa soksi au gloves wakati hujavaa
>>Kuhisi kama vile kuna kitu chenye ncha kali kinakuchoma miguuni au kwenye vidole
HIZI NDIZO SABABU ZA KUDHOOFIKA KWA NEVA HIZO
>>Kupungua kwa virutubisho mwilini. Hapa tunamaanisha mwili kutokuwa na Vitamin za kutosha hasa mkusanyiko wa Vitamini B Complex
>>Matumizi ya dawa fulani kwa muda mrefu mfano TB na ARV
>>Uzito mkubwa wa mwili. Hii hupelekea maumbile ya viungo vya mwili mfano umbile la uti wa mgongo huonekana tofauti na ilivyo kawaida. Kubadilika huku husababisha baadhi ya Neva katika uti wa mgongo zikandamizwe zaidi na misuli/uzito wa mwili na hivyo kusababisha Neva hizo zishindwe kufanya kazi vizuri, matokeo yake unaanza kuhisi maumivu au miguu/mikono kufa ganzi.
>>ugonjwa wa kisukari
>>shinikizo la damu
Hizi ndizo sababu za tatizo hilo, hivyo tusitegemee kwenye mambo ya kishirikina kabisa!!!!
MATIBABU AU USHAURI
1) Kubadili tabia hasa vyakula vinavyochangia tatizo hili.
2) Kutumia virutubisho ambavyo vitaweza kukurejesha katika hali ya zamani
Comments
Post a Comment