ZIJUE FAIDA KUMI ZA ASALI KIAFYA.


 ZIJUE FAIDA KUMI ZA ASALI KIAFYA.


Kwa miaka mingi asali imekuwa ikitumika kiafya kwa ajili ya tiba asili ya magonjwa na matatizo mbali mbali kama maambukizi, kuungua, vidonda, makovu, uvimbe na maumivu.


Zifuatazo ni faida kumi za asali kiafya:-


1. Asali ikichanganywa na maziwa usaidia kupunguza kiungulia.


2. Mchanganyiko wa asali na Limao kwenye chai husaidia kutibu kikohozi na maambukizi kwenye mfumo wa hewa.


3. Mchanganyiko wa asali na tangawizi huzuia kutapika kwa mgonjwa na mama mjamzito.


4. Asali ina kemikali za flavonoid na antioxidants zinazosaidia kuzuia magonjwa ya moyo na saratani.


5. Asali ina kemikali ya hydrogen peroxide ambayo husaidia kuua bakteria na fungasi mwilini.


6. Huwasaidia wanariadha kuongeza nguvu na kupata ahueni mapema kila baada ya kukimbia kwani ina kiasi kikubwa cha glycogen.


7. Asali huongeza kinga ya mwili kwa kuraisisha mfumo wa chakula na damu kufanya kazi vizuri.


8. Mchanganyiko wa asali na juice ya machungwa husaidia kuondoa sumu mwilini na kuimarisha mwili   kwani ina sukari ya asili fructose ambayo husaidia ini kufanya kazi.


9. Huongeza uwezo wa akili kujifunza, kufikiria na kutunza kumbukumbu.


10. Mask ya asali usoni kwa muda wa masaa kadhaa husaidia kuondoa,  kutibu chunusi na kulainisha uso.

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI

ZIJUE FAIDA KUMI (10) ZA STRAWBERRY MWILINI