UWEZO WA STAFELI KATIKA KUPAMBANA NA MAGONJWA SUGU


 UWEZO WA STAFELI KATIKA KUPAMBANA NA MAGONJWA SUGU


@-Stafeli ni tunda lenye faida lukuki kwa afya ya mwanadamu. Zifuatazo ni faida muhimu za mti wa Mstafeli.


@-KWA mfano baadhi ya dawa za hospitali huathiri njia ya chakula na kumsababishia mgonjwa ukosefu wa choo kwa muda mrefu, lakini stafeli likitumika hurekebisha hali hiyo na kumsaidia mgonjwa kupata choo kama kawaida.


@-Vilevile, baadhi ya dawa za hospitali za saratani hudhoofisha kinga ya mwili, lakini virutubisho vilivyomo kwenye stafeli, hasa vitamin C, huzifanya kinga kuwa imara na hivyo kuziimarisha hivyo kumuepusha mtu kupatwa na maambukizi mengine, kama ya njia ya mkojo, mafua na kikohozi cha mara kwa mara.


FAIDA ZINGINE ZA STAFELI NI KAMA ZIFUATAVYO:

Hutoa nafuu ya kipanda uso.

Kirutubisho aina ya Riboflavin kilichomo kwenye stafeli, husadia kutoa nafuu kwa ugonjwa wa kichwa cha kipanda usoni.


1- HUZUIA UGONJWA WA ANEMIA

Madini ya chuma (iron) yaliyomo kwenye stafeli, hufaa sana katika kuzuia ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia).


2-HUTIBU MAGONJWA YA INI

Juisi ya stafeli inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu matatizo ya kwenye ini na uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.


3-HUIMARISHA MIFUPA

Stafeli ni chanzo kizuri pia cha madini ya kopa (copper) na kashiamu (calcium), virutubisho ambavyo huwa muhimu kwa ukuaji wa mifupa mwilini.

Matatizo mengine yanayoweza kudhibitiwa na stafeli ni pamoja na kuumwa miguu, maumivu kwenye ‘joints’, mwili kukosa nguvu na matatizo mengine ya viungo.


4 -MAJANI, MIZIZI, MAGAMBA NAYO NI DAWA

Mbali ya tunda lenyewe kuwa na faida lukuki kama zilivyoanishwa hapo juu, vilivyomo vingine kwenye mti huo kama vile mizizi, majani na magamba yake ni dawa ya magonjwa mbalimbali:


Unywaji wa maji yaliyotengenezwa kutokana na majani ya mstafeli hutibu magonjwa ya ngozi, chunusi na uvimbe wa mwili.

Maji ya majani ya mstafeli pia hutibu ugonjwa wa kuhara, kukohoa, kuvimba miguu, mapunye kichwani. Aidha, maji ya majani ya mstafeli yamethibitika kushusha kiwango cha sukari mwilini.


TAHADHARI

Inaelezwa kwamba stafeli linaweza kuwa siyo salama kwa wajawazito, wagonjwa wa presha ya kupanda au kushuka (hypotension or hypertension), hivyo wanashauriwa kabla ya kula, wapate ushauri wa daktari kwanza.


 USHAURI

Kwa asili yake, stafeli lina kiasi kingi cha virutubisho vinavyoua bakteria, hivyo ulaji wa muda mrefu wa tunda hili kunaweza kuua bakteria wote tumboni hata wale wazuri, hivyo iwapo utalila tunda hili kwa zaidi siku 30 mfululizo, unashauriwa pia kuongezea na dawa za kulainisha njia ya chakula.


 JINSI YA KULITUMIA STAFELI

Stafeli linaweza kuliwa katika aina tofauti. Kama unataka kupata faida zake zote, unaweza kulila lililoiva kama lilivyo au unaweza kutengeneza juisi yake. Unywaji wa maji yatokanayo na majani, mizizi au magamba yake, unaweza kunywa kama chai au kinywaji kingine cha kawaida.

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI