TIBA YA KUKOJOA KITANDANI KWA MTU MZIMA NA WATOTO


 JE,TATIZO LA MTU MZIMA KUKOJOA KITANDANI(ADULTS NOCTURNAL ENURESIS) NI NINI?


Hili ni tatizo linaowasumbua watu wengi walio katika umri ambao tayari wana uwezo wa kuzuia mkojo,tatizo hili hutokea kwa mtu huyo ambaye tayari yupo katika umri wa kuweza kujizuia mkojo ila anakua bado anaendelea kukojoa kitandani au kwenye nguo.

Hivyo tunaweza kusema hili ni  tatizo la kushindwa kuzuia mkojo wakati wa mchana au usiku na linalotokea katika umri wa miaka mitano au zaidi.


Mkojo unapo hifadhiwa katika kibofu cha mkojo, kibofu kinatanuka kama puto. Katika sehemu za neva za kutanua kuta za kibofu cha mkojo zinapeleka ishara ya kuzuia mkojo katika akili.


Hii hutokea katika sehemu ya ubongo inayohusika na matendo yasiyo ya hiari. Kama ubongo wa mtoto haujapata ishara hii, au ukishindwa kujua maana ya hiyo ishara, hatua ya makusudi ya kuzuia mkojo haitafanyika hivyo mtu hushindwa kupata uwezo wa kuxuik mkojo.


Hali hii mara nyingi husababishwa na kuchelewa kwa ukuaji wa kibiologia wa utendaji kazi wa kuzuia mkojo na Ukuaji wa kijinsia unaweza kusababishwa na;


1} Kushindwa kwa akili kutambua ishara kutoka kwenye kibofu cha mkojo,

2} Ujazo mdogo wa kibofu cha mkojo; au 3} Usingizi mzito.

Kwa sasa tafiti zinaonyesha kwamba watu wanaokojoa kitandani ni wagumu kuamka kutoka usingizini kuliko ambao hawana tatizo hilo.


Ni muhimu kutambua kwamba watu hawa hawajikojolei kwa makusudi na kawaida huona aibu kwa sababu hiyo hivyo ukiwa ndugu au mzazi au mpenzi wa mwenye tatizo hili haupaswi kumdhalilisha kwa kumwaibisha au kumtenga bali unatakiwa kumsaidia kupata ufumbuzi wa tatizo Hili.


KADHALIKA TATIZO HILI LA KUJIKOJOLEA LIMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU KUU MBILI. 

YANI 


1)PRIMARY ENURESIS 

Aina hii ni pale mtu anaposhindwa kuwa na uwezo wa kuzuia mkojo tangia utotoni kwake,


2)Secondary enuresis

Aina hii ni pale mtu anaweza kujizuia kujikojolea kwa miezi sita au zaidi, halafu anaanza kujikojolea tena.


Mpendwa msomaji katika aina hiyo ya  kwanza yani PRIMARY ENURESIS hili ni tatizo la kurithi na huwapata watu wa familia moja. 


KADHALIKA TATIZO HILI LIMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU MBILI. 

1. Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku (NOCTURNAL ENURESIS) na lile la mtu kujikojolea wakati wa mchana (DIURNAL ENURESIS). Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku huonekana zaidi kwa watoto wa kiume na lile la kujikojolea mchana mara nyingi huwa kwa wasichana.


CHANZO CHA TATIZO

Mpendwa msomaji utafiti umeonyesha kua kuna sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili la kukojoa kitandani na miongoni mwa sababu hizo ni


1)OVERACTIVE BLADDER (OAB)

Hili ni tatizo la kibofu cha mkojo kuruhusu mkojo kutoka kwa ghafla bila ya muhusika kuwa na utayari na hivyo hukosa uwezo wa kujizuia kujikojolea,hali hii husababisha mtu kuonekana amejikojolea pasipo kujitambua.


2) STRESS (Msongo mkali wa mawazo )

Kwa upande mwingine tatizo la kukojoa kitandani huweza kuwa limesababiswa na matatizo ya hisia au ya kisaikolojia na msongo wa mawazo(stress).


3)MADAWA

Kuna baadhi ya dawa husababisha mtu kupatwa na hali ya kujikojolea dawa hizo ni za usingizi na dawa zinazotumika kutibu magonjwa ya akili mfano wa dawa hizo ni

Clozapine,cariprazine, risperidone etc


4) TATIZO LA KUKOSA HAJA KUBWA (CONSTIPATION)


5) KISUKARI (DIABETES)


6) MATATIZO YA FIGO (KIDNEY DISEASES)


7)TEZI DUME (ENLARGED PROSTATE)

8)MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO(URINARY TRACT INFECTION)

9)TATIZO LA KUFUNGWA KWA NJIA ZA HEWA WAKATI WA USINGIZI (OBSTRUCTIVE SLEEP APNEA)

10) KIBOFU CHA MKOJO KUWA KIDOGO(SMALL BLADDER)


VIPIMO NA UCHUNGUZI


@-Ni mara ngapi na kwa wakati gani huwa unajikojolea (je,ni usiku au mchana)?


@-Kiasi gani mkojo hukutoka (mwingi au kidogo)?


@-Ni kiasi gani cha vinywaji ulikunywa kabla ya kupanda kitandani?


@-Dalili zingine zozote ambazo umekuwa nazo(unahisi maumivu baada ya kutokwa na mkojo)?


@-Iwapo daktari wako atahitaji zaidi Kukufanyia uchunguzi ataagiza vipimo vifuatavyo÷


A-URINE CULTURE AND URINE ANALYSIS : Vipimo hivi hutumika kuangalia maambukizi, damu isiyohitajika na vitu vingine kwenye mkojo.


B-BLOOD TESTS : kipimo hiki cha damu hutumika kuangalia figo na tezi, kiwango cha cholesterol iliyopo katika damu na iwapo kama Kuna shida ya upungufu wa damu au ugonjwa wa kisukari na homoni.


C-BLADDER SCANS : hiki ni kipimo cha ultrasound ambacho mgonjwa atatakiwa kupima ili tujue ni kiwango  gani cha mkojo hubakia katika kibofu mara baada ya kukojoa.


D-URODYNAMIC TESTS : kipimo hiki kitahitajika kupimwa ili kuangalia au kuona jinsi sehemu ya chini ya mkojo huhifadhi na kutoa mkojo kiwango gani


E-CYSTOSCOPY : kipimo hiki pia kitahitajika kuhitimisha uchunguzi ambapo daktari ataingiza bomba nyembamba na lens ndogo ndani ya kibofu cha mkojo ili kuangalia iwapo kuna dalili ya uvimbe,kansa na matatizo mengine.


MATIBABU 


Mpendwa msomaji napenda kuhitimisha somo langu hili kwa kukusihi iwapo una hili tatizo au ndugu yako analo tafadhal fahamu kuwa tatizo hili lina matibabu mengi ambayo matibabu haya hutofautiana kwani mengine hufanya kazi vizuri zaidi ya matibabu mengine.


MATIBABU YANAYOHUSU MFUMO WA MAISHA(LIFESTYLE TREATMENT)


Aina hii ya matibabu inajumuisha kubadilisha ama kudhibiti baadhi ya mambo yaliyopo katika maisha ya muhusika ili kuweza kupona  tatizo hili,miongoni mwa hayo mambo ni


1-Kudhibiti utumiaji wa vinywaji


2-Kuwa na ratiba ya kuamka usiku:

 

3-Kuwa na ratiba ya kwenda chooni mara kwa mara wakati wa mchana; 


4-Epuka vitu vinavyofanya kibofu cha mkojo kujaa kwa haraka 


 MATIBABU YANAYOHUSISHA DAWA (MEDICINE)

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI

ZIJUE FAIDA KUMI (10) ZA STRAWBERRY MWILINI