JIFUNZE JINSI YA KUTIBU MAUMIVU YA SIKIO KWA KUTUMIA KITUNGUU SAUMU
JIFUNZE JINSI YA KUTIBU MAUMIVU YA SIKIO KWA KUTUMIA KITUNGUU SAUMU
Tatizo la kuumwa sikio linajitokeza mara kwa mara katika jamii zetu, ni tatizo lakawaida lakini huwa hatari zaidi hasa pale tiba inapopuuzwa au kucheleweshwa
SABABU ZAKE
Miongoni mwa sababu za kupata maumivu makali ya sikio ni:-
1. Maambukizi yatokanayo na bakteria, fangas, virus n.k
2. Kubadilika kwa mkandamizo wa presha(pressure changes) kwenye masikio mfano wakati wa kuogelea na shughuli zingine
3. Maji kuingia masikioni
4. Hali ya hewa iliyoptiliza
5. Kuchokonoa masikio
TIBA
Menya kitunguu saumu kisha kamua juice yake, ipashe moto kiasi kisha itumike ikiwa bado ya vuguvugu. Usichanganye na maji
DOZI
Dondoshea matone 2 - 3 ya mafuta hayo(juice) katika sikio lenye tatizo kisha weka pamba ama kitambaa safi kwa muda wa dakika 30 kufanya dawa iendelee kuwepo sikioni.... Fanya hivyo kwa muda wa siku 2 hadi 3 tatizo litaisha
ZINGATIA
1. Tumia dawa ikiwa ya vuguvugu(sio ya moto sana wala baridi sana)
2. Usitumie dawa hii kwenye sikio linalotoa usaha wala majimaji yeyote
● Kitunguu saumu kinatumika pia kutibu uvimbe(ant-imflamatory), maambukizi ya bakteria na fangasi.
Comments
Post a Comment