FAHAMU KUHUSU KAROTI NA FAIDA ZAKE KIAFYA
SOMO LETU LEO TUNAJIFUNZA KUHUSU KAROTI.
karoti ni moja wapo kiungo watu wanatumia karoti kuungia mboga na wengine wanatumia kutafuna tu lakini sina uhakika kama watu wanajua umuhimu wa karoti kwa afya zao
👉Wataalamu wa tiba asili namimi nikiwemo wanashauri kuwa hili uwe na afya bora inabidi ule karoti 6 kwa wiki. Unaweza kula karoti kwa kuchemsha_
Kula mbichi au kunywa juce yake.
👉karoti husaidia kuondoa tatizo la macho kutoona vizuri usiku pia inasaidia kuondoa tatizo la #ALLERGY kwenye macho_
Mfano macho kuwasha sababu ya vumbi au moshi.
👉karoti inalekebisha seli mwilini na kuzifanya zisizeeke mapema hii ni kutokana vitamin A) iliyopo kwenye karoti.
👉karoti huifanya ngozi iwe nzuri na yenye kupendeza_
Kama unataka kutumia karoti hili kufanya ngozi yako ipendeze iwe laini chukua asali mbichi kijiko 1 cha chakula na mafuta ya mzaituni (olive oil) kijiko kimoja cha chakula na maji ya limao kijiko kimoja vyote ivyo unachanganya kwenye juisi ya karoti nusu glas_
Changanya mchanganyiko wako vizuri kisha tumia sugua taratibu sehemu yoyote ya ngozi unayotaka ipendeze kisha kaa kama muda wa dakika 15 ndo uwende kuoga au kunawa kwa maji ya kawaida tiba hii ni nzuri sana itakusaidia kuondoa chunusi mba,mabaka, na kuondoa madoa doa kwenye ngozi yako.
👉karoti husaidia kuondoa sumu (taka) mwilini na kuondoa mafuta yasiyotakiwa mwilini na kusafisha njia ya haja kubwa na kusaidia kupata choo vizuri.
👉karoti zinasaidia fizi na meno kuwa amara na kuchochea uzalishaji wa mate.
👉karoti inasaidia kuzuia kiharusi utafti unaonyesha kuwa ulaji wa karoti 6 kwa wiki husaidia kutopata kiharusi.
👉karoti husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu.
👉karoti husaidia tatizo la kupoteza kumbu kumbu. (Kusahau)
👉ulaji wa karoti 6 kwa wiki zinasaidia kutopata ugonjwa saratani bi maana karoti zinatumika kama kinga ya ungonjwa wa saratani na ugonjwa wa kisukari. Nk..
👆hizo ndo faida za kula karoti. Tujitahidi sana kula angalau karoti 6 kwa wiki
Comments
Post a Comment