FAIDA ZA TUNDA LA KARAKARA (PASSION)
FAHAMU FAIDA ZA TUNDA LA KARAKARA (PASSION)
Pia tunda la karakara si zuri kwa Wajawazito na Watoto
KARAKARA (Passion) ni tunda linaloota katikq mmea unaosambaa ambao wakati mwingine huwekewa mti ili usambae vizuri na kutoa matunda mengi.
Asili ya tunda hili ni Amerika ya kusini ambapo inaaminika kuwa kwa Mara ya kwanza mmea wake ulipandwa nchini Hawaii, mwaka 1880.
Kwa hapa Tanzania Mmea wa Karakara (Passion) hupandwa sana maeneo ya Morogoro, Kigoma, Dar es salaam, Tanga, Arusha, Pwani na Visiwani Zanzibar.
Tunda hili linavirutubisho mbalimbali katika mwili wa binadamu. Virutubisho hivyo ni pamoja na Vitamin A, C, B2, B6 na E, Flavonoids, pamoja na madini ya chuma.
FAIDA ZA TUNDA LA KARAKARA (PASSION)
__ Hupunguza maumivu ya mishipa ya fahamu na tumbo la hedhi kwa akina mama.
__ Hutibu matatizo ya wasiwasi, msongo wa mawazo na hali ya kuzubaa kwa wazee na watoto.
__ Huboresha Afya ya mifupa kutokana na kuwa na madini ya Magnesium, Copper, Phosphorus.
__ Kwa Mtu anayesumbuliwa na U.T.I anashauriwa kutumia tunda hili Mara kwa Mara kwa husaidia kuondoa tatizo hilo.
__ Ulaji wa matunda haya ya karakara (Passion) mawili au matatu kwa siku pamoja na nyama zake za ndani husaidia kuupa mwili nyuzinyizi (fibres), Calcium na Vilainishi muhimu ambavyo husaidia kuondokana na tatizo la Ukavu Mavi au kupata choo kwa shida (Constipation).
Hata hivyo watafiti wanasema kuwa, wajawazito na watoto wachanga wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotumia tunda hili. Hii ni kutokana na katika majaribio ya utafiti huo walibaini matunda hayo yana uwezo wa kusababisha uchungu hivyo kujikuta wanajifungua kabla ya wakati, lakini pia huweza kusababisha usingizi hivyo si vizuri kwao kulitumia.
Comments
Post a Comment