MWANAUME WAJUE MAADUI 20 WA UUME WAKO

MAADUI 20 WA UUME WAKO

1.MAGONJWA

Magonjwa ni adui namba 1 wa uume wako.
Magonjwa ya sehemu za siri, magonjwa ya mwili kwa ujumla, na magonjwa ya wanaume kama - tezi dume ni adui wa uume wako. Ugonjwa kama kisukari na presha, figo na ini kutokufanya kazi vizuri LAZIMA uume uwe dhaifu. Kuna magonjwa mengine pia kama viupele vya ajabu ajabu huko kwa babu pamoja na ugonjwa wa bawasiri.
MAGONJWA HAYA LAZIMA YATIBIWE HARAKA.

2. ULEVI NA SIGARA

Ulevi haufai kabisa kwa afya ya uume wako. Ulevi unakufanya uwe mlaji wa nyama hasa nyekundu, unakuwa sio mwepesi wa kunywa maziwa na kula matunda, unakuwa mzembe wa majukumu yako ya ndani, unapata vitambi, unaharibu balansi ya homoni.  unaelekea upotevuni.

Kunywa maji ya kutosha, maji fresh ili kuuburudisha mwili na kuondoa msongo wa mawazo.

3. PUNYETO NA MICHEPUKO

Watu walionishuhudia ambao walifungwa katika minyororo ya kufanya punyeto hadi mara 6 kwa siku, waliokuwa wanafanya hadi vyoo vya ofisini na wengine kujificha hata majumbani wake zao wakiwa wamelala au hawapo. Vijana wa boarding school na vyuo, mabachela na wengineo wanatoa shuhuda zinazotisha. Punyeto imekuwa utumwa.
Wanashuhudia kupata majipu, michubuko,
msongo wa mawazo, kushuka kwa kujiamini,
wengine wameshuhudia kufika kiwango cha juu cha kutokuvutiwa na wanawake kabisa.

Kwa kifupi punyeto huharibu vipokezi (receivers) vya hisia mwilini na saikolojia yako ya mapenzi kwa ujumla, kuharibu mishipa na nerve za ufahamu katika uume na kukukosesha mawasiliano sahihi kati ya uume na akili yako. Unaporudi kufanya
tendo la ndoa kawaida (na mwanamke) unakuwa tayari umeathirika na inakuwa kama upo ulimwengu wa nje ya mapenzi. Wengine wanasema haina madhara na pia kutoa namna nzuri ya kufanya ili usipate madhara, lakini kila waathirika wanasema haifai….kinga ni bora kuliko tiba hivyo anza mpango wa kuacha punyeto haraka kabla hujafikia sehemu mbaya zaidi.

4. MADAWA

Hapa kuna madawa ya kulevya na madawa ya kawaida, pia madawa makali ya presha na
kisukari ni hatari kwa afya ya uume wako.
Madawa yanayowekwa katika baadhi ya makopo ya vyakula vilivyosindikwa na mengine yanayonyunyiziwa mashambani wakati mimea inakuwa katika ukuaji wake ni hatari tupu.

Madawa ya kulevya nadhani wote tunayajua
yalivyo noma. Unalegea mwili mzima, uume
unajifia tu kama bamia. Jenga tabia ya kutumia chakula cha asili kama dawa kuepuka magonjwa ya tabia yasikupate.

5. UCHAFU WA MWILI NA NGUO ZA KUBANA

Nguo chafu, za mbano na zisizo za pamba
zinasababisha magonjwa ya ngozi. Pia uume
unatakiwa upate free range yaani ubembee na sio kutulia kama jiwe. Hii inaufanya uume kuwa active na kuwa tayari kwa kushughulika. Pia wanaume wengi ni mabingwa wa kuvaa suruali si chini ya siku 3 hadi 7. Wengine wanavaa jinsi kauka nikuvae - huo ni uchafu na ni hatari uchafu kuingia ikulu. Oga mara kwa mara fua nguo zako
hata kama wife hafanyi fanya mwenyewe, vaa boxer chupi sio zile za chupi za V kama za wanawake. Ukikojoa na kwenda haja kubwa jitawaze vizuri. Kuwa msafi mwili na roho, Sasa wengine wanafuga rasta maeneo ya Ikulu. … OK decide yourself kama ni usafi huo au uchafu.

6. BAADHI YA CHAKULA

Hapa lazima tuambiane ukweli ivi mwanaume unakula chips na soda kila siku unataka uwe nini kama sio kituko, vyakula vyepesi vyepesi visivyokuwa na nguvu vinavyokuongezea sukari na presha mwilini achana navyo. Mwambie waifu
aachane na mapishi ya ugali uliokobolewa.
Vyakula vya kukujaza gesi tumboni havifai,
vyakula vinavonenepesha tumbo achana navyo kabisa. Wengine wanapiga pombe kali eti zinaongeza nguvu, at least kwa leo au kesho “energy drinks is not a long lasting solution”.
Mara moja moja penda kutumia asali na
mdalasini, tende, matunda kwa wingi hasa yale yenye zink kama tikiti maji, avocado, uyoga na pia machungwa. Hakikisha unakula matunda dakika kadhaa kabla au baada ya chakula. Usichanganye matunda yenye acid na alkali mara moja na ukala yaani mtindo wa cocktail, mfano chungwa lina acid, parachichi ni alkaline (haya usiyale yote
mara moja).

7. HOMONI KUVURUGWA

Hapa ndugu zangu pana uhusiano sana na
namba 4 hapo juu. Vyakula na madawa
tunayotumia pamoja na madawa yaliyotumika na wakulima ndio yanaleteleza homoni katika mwili wako kuwa na balansi ya tofauti. Matokeo yake homoni zinazohitajika kuamsha vichocheo vya kuufanya uume ufanye kazi vema zinashindwa kuwa katika balansi nzuri na hatimaye kuufanya uume kushindwa kufanya kazi zake kwa ufasaha.

8. UMRI

Kadri umri wako unavozidi kwenda mbele ndivyo uwezo wa kiafya wa uume wako unavyozidi kupungua ingawa wanasema "old wine gets better" Magonjwa pia ni rahisi kukuingia, magonjwa kama tezi dume, kansa ya uume, ubovu wa kibofu cha mkojo na pia kukosekana kwa damu katika sehemu zako za siri.

9. KUUCHORA UUME KWA KUTOBOA
AU KUPAKA RANGI

Wanaume wengine hujichora katika uume wao na kuweka alama mbalimbali au majina mbalimbali. Kwa kuwa kazi hizi katika mazingira ya kiafrika hufanywa kwa siri basi vitogeo huwa dhaifu na huenda vikaambukiza magonjwa, lakini pia ukishachora uume wako kwa kutoboa ngozi ni rahisi kwa magonjwa kukuingia wakati ukiwa katika harakati zako za kinyumba.

10. ACROBATIC AND ATHLETIC SEX

Hawa pia ni maadui wakubwa, kuna baadhi ya wanandoa hufanya mapenzi kwa kutumia staili za tofauti tofauti na zingine huufanya uume kupenya kwa shida au kukunjana na hivyo kusababisha michubuko na uvimbe katika kichwa na shingo ya uume. Na pia wengine hufanya mapenzi muda mrefu sana kama vile wako mashindanoni -
Jiulize unabakia salama? Starehe isiwe kero.
Pima faida ya starehe na hasara yake.

11. MSONGO WA MAWAZO

Huyu ni adui endapo utashindwa kumdhibiti kwa kuwa stress husababisha milango ya fahamu kuziba na pia kuunyima uume damu
na oxygen ya kutosha na hivyo uume kushindwa kufanya kazi yake vizuri. Ikiwa utashindwa kuusimamisha uume huenda ukashindwa mara nyingine tena kwa kuwa swala hilo linaweza kuathiri saikolojia yako ya mapenzi na hivyo kujikuta kila wakati unashindwa wakati ki-ukweli upo fiti. Jifunze kuwa nje ya stress kama vile kupangilia mambo yako vizuri ya kijamii, kiofis na
kipesa (kwa sababu stress au msongo hutokea wakati matokeo halisi yamekuwa madogo kuliko matokeo tarajiwa na inaonekana hamna namna ya kufanya na muda umekwisha) – Siku zote panga siku yako vizuri na yaangalie mambo yote
kwa kutumia akili chanya. Katika kila ubaya kuna uzuri, fuata uzuri.

12. NGONO KINYUME CHA MAUMBILE,
VIDOLE NA MIDOLI

Ufanyaji ngono kinyume na maumbile ni hatari kwa afya ya uume wako, iwe unafanya au unafanywa yote yanapelekea kuwa na hali ya sintofahamu mara uume unapokutana na uke. Sio mazoea yake na sio utaratibu wa dini zetu hata wapagani wanakataa wala sio uhalisia. Wengine wana vimidoli vyao na vitu vinavyofanana na hivyo. Unasinyaisha uume wako….mtoto wako anapokuwa na tabia za ajabu ajabu mkague na uongee naye mara kwa mara sio kila siku unarudi watoto wamelala.

13. WASIWASI, WOGA NA UVIVU
WAKATI NA KABLA YA TENDO LA NDOA

Hapa ndugu zangu hakuna maelezo mengi sana ila kumbuka tu ya kwamba kuwa na wasiwasi na woga kunaondoa uwezo wa damu kufika maeneo ya uumeni hivyo kuukosesha uume malighafi muhimu ya damu na oxygeni ili uume ufanye kazi
vizuri. Pia wewe mwenyewe mwanaume unakosa focus (target) ya jambo unalolifanya. Kuwa mwanaume jiamini unaweza.

14. UPUNGUFU WA TESTESTORENE

Testosterone ndio homoni ya kiume inayohusika na uundaji wa viungo vya kiume wakati mtoto akiwa tumboni hajazaliwa na kisha kuanza kujenga mwili wa kiume wakati kabla ya kubalehesha na kumtayarisha kijana wa kiume kuwa baba akisha balehe. Na baada ya hapo homoni hii huhusika na matendo mabalimbali ya kimapenzi na mvutano kati ya mwanamke na mwanaume. Pia huhusika na uzalishaji na ukomazaji wa mbegu za kiume. Homoni hii ikipungua uwezo wa uume kufanya kazi vizuri
hupungua. Uzuri ni kwamba unaweza kuongezwa homini hii katika mahospitali lakini pia kuna vyakula unavyoweza kula na kuiongeza taratibu.

15. PICHA CHAFU, ROHO CHAFU NA
AKILI CHAFU

Uangaliaji wa picha chafu za ngono ni hatari kwaujumla wa saikolojia yako. Mwili wako una uwezo wa kubadili tabia na vionjo kama utafanya hivyo ndani ya siku 15 hadi 21. Ikiwa utazoea kuangalia picha za ngono ambazo wataalamu wengi wa hollywood wanasema si za kweli basi unajikuta upo katika ulimwengu ambao sio halisia. Ukija
kuonana na mkeo halisi unajikuta mwili wako wa hisia bado upo Hollywood. Akili yako imetekwa.
Huwezi fanya vizuri tena, wengine wanasema
wanatafuta apetite, lakini kumbuka apetite hii sio ya asili baada ya muda unazoea unakuwa sugu na huwezi tena kuwa boosted na hizo picha. Best apetizer ni mkeo.

16. MWANAMKE MWENYE DHARAU NA
MATUSI

Tabia za baadhi ya wanawake zimekuwa kero kabisa kwa uimara wa uume. Mwanamke anakuwa mchafu kupindukia. Wengine ni kutoa matusi mfululizo kama vile hawajaenda jandoni, wengine ni dharau zisizokuwa na mpango hadi wakati wa tendo la ndoa. Wanawake wengine hawachangamki hata mwanaume ajitahidi vipi yaani wapo wapo tu as if ni magogo. Hii ni hatari sana. Mwanamke ni ufunguo mzuri sana kwa afya ya mwanaume hasa kama mwanamke ameutunza vizuri uke wake na pia kama mwanaume hajaathirika na uoga, wasiwasi na mashaka, magonjwa na tabia zile mbaya kama punyeto, michepuko, ulevi na madawa ya kulevya. Wewe mwanume unatakiwa utengeneze mazingira ya mkeo kuwa msafi na mwema kwako, anayejituma
na ambaye ni mkweli daima. Love your wife she will pay you back 100%.

17. UZITO, KITAMBI NA KIRIBA TUMBO CHA MWANAMKE

Wanawake wengi siku hizi wana vitambi, owk unaweza sema hii inakujaje hapa? Ukweli ni kwamba baadhi ya shughuli za msingi za uume zinashindikana kufanyika kwa sababu ya kitambi cha mwanamke, ofcourse hata kitambi cha mwanaume ni adui lakini adui namba moja ni kitambi cha mwanamke na pili ni kitambi cha mwanaume. Wanawake wengi wanaoshindwa kufika kileleni wanavitambi au uzito mkubwa. Hii inauletea uume shida sana ya kutimiza majukumu ya kinyumba.

18. UKE USIOTUNZWA.

Uume unakuwa bora ikiwa uke pia ni bora.
Mwanaume lazima ujiunge na mkeo kumweka vizuri.

19. KUKOSA USINGIZI

Kuangalia mpira kuanzia saa11 mpaka saa7
usiku, wengine wanaangalia movie huku wanakula mirungi na bado asubuhi unatakiwa uwahi kazini. My friend unaharibu mwili wako na uume wako unapata stress. Ukilala mwili unapata muda wa kurekebisha misuli, kuweka balansi nzuri ya homoni na kurudisha hamu za mwili za kawaida pia kuboresha kinga ya mwili. pata usingizi wa kutosha ubongo ujipange,misuli itulie na seli zizaliane.

20. TOO MUCH SEX IS HARMFUL.

Ukifanya sana ngono una hatari ya kupata
madhara yafuatayo uume kuvunjika (hauvunjiki kama kijiti ila misuli inaumia), kuishiwa maji mwilini, UTI, kuumiza nerve za uume, kupunguza nguvu ya misuli na kushindwa au kuuma misuli ya mwili. AMUA NI KIASI GANI KINAFAA.

Kwa ujumla utakuwa umegundua ya kwamba
chakula ndio suluhisho la kudumu la kupambana na maadui hawa, ingawa pia utalazimika kuwa mwenye tabia nzuri. Endapo wakati mwingine inakuwa ngumu kwa chakula kufanya kazi na kuleta matokea ya haraka itakulazimu kupata ushauri wa kitabibu kama kupata dawa za hospitalini (kemikali) au virutubisho. Ikiwa utapata dawa au virutubisho hivi na ukapona huna budi kuendelea kutumia chakula bora na pia kuwa na tabia njema kwa ajili ya kupata matokeo ya kudumu, yenye furaha na amani.

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI