JINSI YA KUMSAIDIA MAMA MJAMZITO ANAYETAPIKA MARA KWA MARA..

Tunamsaidia vipi mama mjamzito anayetapika mara kwa mara...!?a la kihomoni jambo ambalo huwafanya wajawazito kuwa mabadiliko pia km kuchukia baadhi ya harufu, watu au aina fulani za vyakula, wengine huwafanya kutapika na kupoteza hamu ya kula jambo ambalo hupoteza virutubisho vingi katika mwili na kupoteza maji mengi.

Dondoo hizi naomba zikusaidie wewe mjamzito na wewe unayeweza kumsaidia mama mjamzito popote ulipo ili kumlinda mama na kiumbe chake...

•Mama mjamzito ale mkate mkavu mara baada ya kuamka asubuhi na maji ya uvuguvugu.

•Mjamzito ale chakula kidogo kikavu usiku

•Mjamzito epuka kula kiasi kikubwa cha mlo badala yake kula vitafunwa au tunda kila baada ya saa moja au mbili na kunywa juisi fresh za matunda na maji sio chini ya lita moja kwa siku

•Kula vyakula vyenye protini kwa wingi, kama karanga, matunda kama papai, chungwa, parachichi, tufaa, vyakula vya nafaka, mayai ya kuchemsha, maziwa mtindi n k

•Mama kijacho Epuka vyakula vyenye chumvi nyingi, sukari nyingi na vile vya kukaushwa kwa mafuta mengi.

•Mama Kija,,,, Kula tangawizi mbichi, au biskuti za tangawizi, chai ya tangawizi au pipi za tangawizi ukihisi hali ya kichefuchefu

•Jitahidi kutapika nyongo wakati wa asubuhi na unaweza kukaa kwa amani mchana kutwa.


Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI