πŸ’žπŸ’ž MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA πŸ’žπŸ’ž


Maumivu wakati wa tendo la ndoa (DYSPAREUNIA) si tu huharibu mudi bali hupelekea kumfanya humusika kuchukia/kuogopa tendo lenyewe, kukosa hamu ya tendo lenyewe na kukosa mashirikiano. Maumivu wakati wa tendo au baada ya tendo ni tatizo kubwa linalowasumbuwa baadhi ya wanawake na wanaume ila ukiona ufanyapo tendo La ndoa na kuhisi maumivu basi juwa mwili wako unakupa ishara ya kwamba kuna kitu hakipo sawa na nivizuri kujichunguza ili kujuwa tatizo.

πŸ’—πŸ’–Zifuatazo ni hali zinazopelekea kusababisha  na namna ya kulitatuwa hilo tatizo


πŸ’•Kutofanyika maandalizi ya kutosha.   Mwanamke kupata hamu huchukuwa muda sana kuliko mwanaume hivo kunatakiwa kuwepo muda wa kutosha ktk suala zima la kutomesana(oral sex), Sio dakika 5 ukishaona majimaji kidogo na kuanza tendo La ndoa hali hii hupelekea kutokea maumivu na kumfanya mtu kuchukia tendo. Unapomuandaa mwenzio vizuri hupelekea damu kutembea vizuri ktk genitals na kufanya kuongezeka majimaji ktk uke (lubrication) yatakayopelekea kulainisha misuli ya uke ili iweze kuhimili uume vizuri.

πŸ’•Ukavu wa uke (vaginismus), hali hii husababisha na utumiaji wa shampoo/sabuni katika uke(vagina) au kwa wengini ni maumbile yao walivoumbwa. Ukavu wa uke hupelekea maumivu makali wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo kwani misuli ya ndani na inayozunguka uke hujifunga na kukaza. Hivo kuepukana na tatizo hili mara nyingi hushauriwa kutumike gel(lube) maalum ili kulainisha eneo husika au unaweza kutumia mafuta ya Nazi original sio feki.

πŸ’•Ukubwa wa uume(penis). Hii pia ni sababu moja wapo inayopeleke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hivo mara nyingi hushauriwa kuwepo na gel(lube) ili kuwepo urahisi wa kupanuka eneo husika uke.

πŸ’•Kuuguwa maradhi ya YEAST INFECTION na SEXUALLY.  TRANSMITTED.  INFECTION (S. T. I). Mwamamke/mwanaume ambae anasumbuliwa na magonjwa yaho lazima atapata maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo kwani kunakuwa na michubuko ktk sehemu zake za siri. Uepukana na tatizo hili ni vizuri ukaonana na dactari kwa uchunguzi zaidi.

πŸ’•Mikao(style) wakati wa tendo la ndoa. Mara nyingi sana huwa tunapanda kujaribu vitu tofauti tofauti na hupelekea kupatwa na maumivu wakati wa tendo. Mfano unaweza ukawa umekaa style ambayo uume(penis) unapoingia basi moja kwa moja unagonga kuta za kizazi na kufanya usikie maumivu.

πŸ’•Msongomano wa mawazo. Kwanza tujuwe akili na mwili hufanya kazi pamoja, kama utakuwa na mawazo basi mwili nao utakuwa hauleti ushirikiano wowote ule hivo kutakosekana majimaji ktk uke na kupelekea kusababisha maumivu makali. Kuepukana na tatizo hili unashauriwa kuweko relaxation ya kutosha.

                         πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI