FAIDA 14 ZA MAEMBE KIAFYA.

FAIDA ZA MAEMBE KIAFYA.


 Maembe ni matamu sana kiradha na hupendwa na watu katika hali toauti.
Mtu anaweza akawa mgonjwa lakini hamu yake ikawa ni maembe kwan wakat mwingine huwa yanarudisha hamu ya kula pale ujisikiapo mgonjwa na kukosa hamu ya chakula.


 FAIDA ZA KIAFYA ZA MAEMBE NI HIZI.


 1. Husaidia sana katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
 Huongeza nguvu katika usagaji wa chakula tumboni.



 2. Huzuia na kupambana na saatani/ kansa.
 Hii ni kwa sababu maembe huwa na viua sumu kama quercetin, fisetin, astragalin, gallic acid, methyl gallate na isoquercitrin ambazo hupambana sana na kansa ya matiti, colon cancer na prostate cancer/kansa ya kibofu.



 3 Husawazisha kiwango cha cholesterol/lehemu kuwa katika mstari usio na hatar ya kupata kisukari.
 Kumbuka hii pia ni kaz ya majani ya maembe. Uwepo wa vitamin C, fibres/kamba au nyuz lishe na madini kama chuma/iron. Chuma majani sita hadi tisa, chemsha kunywa asubuhi kabla ya kula chochote.



4. Kuongeza uzito mwilini na kuimarisha afya ya mifupa.
 Maembe yana vitamin K ambayo huwezesha uvutwaji wa madini ya calcium.



5. Afya ya macho.
 Huongeza uwezo wa kuona kutokana na madini na vitamin zake.



 6. Afya ya moyo.
 Huupa afya moyo kwasababu ya fibre/kamba lishe na vitamin.



 7. Afya ya ngozi na nywele.
Kuwa na vitamin A ambayo hufanya kazi yake mwilini.



8. Afya ya mama mjamzito.
 Mama mjamzito anashauriwa kutumia maembe kwan yana madini chuma/ iron ambayo husaidia mjengo wa mifupa na misuli kwa mtoto.



9. Maembe huzuia Pumu/ asthma.
Yana kiwango kikubwa cha betacarotene.



10. Huupa nguvu mfumo wa kinga mwilini dhidi ya magonjwa.



11. Sifa ya kupinga ukuaji au uzeekaji wa haraka.



12. Maembe kwa ajili ya kumbukumbu na uwezo wa kudaka vitu kichwani/kuelewa.



13. Maembe ambayo hayajaiva sana husaidia kupunguza kichefuchefu.



14 Juice ya maembe kwa urembo.
 ukiweka na asali kidogo changanya, weka mask usoni pia sugua/scrab na uoshe kwa maji safi. Ngozi itafurahi.


Hakikisha Unathamini Afya Yako

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI

ZIJUE FAIDA KUMI (10) ZA STRAWBERRY MWILINI