FAIDA 13 ZA TANGO (CUCUMBER).

ZIPO FAIDA 13 ZA TANGO (CUCUMBER).



Mara kadhaa tumekua tukitumia Tango kama moja ya matunda yetu. Lakini je umepata kujua kazi za Tango mwilini? Makala hii itaangazia faida kedekede za Tango katika mwili wa binadamu. Wengi wetu tumekua tukila matunda kwa kupenda ladha yake lakini hatujapata bahati ya kujua kwa undani faida za matunda hayo.

Awali ya yote ni vyema kutambua ni tango lipi linafaaa kwa kula?

Tango linalofaa kwa kula ni tango lenye rangi ya kijani iliyokolea na lisilo tepeta, tango la aina hii ni zuri zaidi.

FAIDA ZA TANGO.

1. Tango husaidia kuupatia mwili maji.
Sehemu kubwa ya tunda hili ni maji hivyo basi husaidia kurejesha maji mwilini.

2. Kupunguza sumu mwilini.
Kutokana upatikanaji wa maji mengi kwenye tunda hili hvo basi ni rahisi kwa maji haya kusaidia zoezi la kuondosha taka mwilini.

3. Chanzo cha vitamin B.
Madini ya silca yapatikananayo kwenye tango husaidia kucha na nywele kung`aa pia kuna madini ya silcon na sulfur kwenye tunda  hili madini haya  husaidia kuondoa uvimbe kwenye ngozi hivyo basi huweza kutumika kama urembo au kwa matunzo ya ngozi.

4. Huondoa harufu mbaya mdomoni.
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa tatizo hili hutibika kabisa kwa kutumia tunda hili. Chukua kipande cha tango kisha kibane kwenye pembe ya kinywa chako kwa muda wa dakika 2 hadi 3 hivi.
Hii itasaidia kuua bakteria wasabaishao harufu mbaya mdomoni kwani tango lina pythochemicals zenye uwezo wa kuua bakteria hao.

5. Tango husaidia kupunguza kiasi cha URIC ACID mwilini hvyo kuliacha figo katika hali yake ya kawaida.

6. Tango hupunguza tatizo la kisukari na kurekebisha shinikizo la damu.
Hii ni kwa sababu, tango lina madini ya potasium na magnesium ambayo ni hitaji kubwa la moyo ili ufanye kazi ipasavyo.

7. Kupambana na kansa ya shingo ya kizazi, kansa ya titi, tezi dume na nyingine nyingi.
Tafiti zinadhihirisha kua tango linauwezo wa kufanya yote haya kutokana na uwepo wa viini lishe kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol.

8. Je, umekua ukisumbuliwa na tatizo la Hang Over?
Tango ni suluhisho la tatizo hili kula vipande kadhaa kabla ya kulala na utaamka ukiwa safi kabisa bila kusumbuliwa na kichwa tena.

9. Husaidia kuimarisha kinga ya mwili, zaidi ya hapo pia Matango yana vitamin A, B na C.

10. Kupunguza uzito.
Tango lina maji kwa wingi hivyo ni moja kati ya vyakula vyenye low calories  ambavyo husaidia kupunguza uzito wa mwili.

11. Kuimarisha mfumo wa mneng’enyo wa chakula.
Hii ni kutokana na uwepo wa fibres pamoja na maji mengi kwenye tango hivyo basi husaidia kuondoa tatizo la kupata choo kigumu.

12. Kutokana na kuwepo kwa maji mengi pamoja na virutubisho mbalimbali kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapokuwa imepanda.

13. Afya ya viungo.
Tango husaidia kupunguza tatizo la ugonjwa wa viungo #gout na ugonjwa wa baridi yabisi Arthritis.

Tango ni moja kati ya matunda yenye kiwango cha juu cha silica ambayo pia kusaidia kuimarisha afya ya viungo mwilini.

Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium hufanya tango linapochanganywa na EXTRA VIGIN FLOUR (inapatikana health and beuty room tz)huweza kutibu gout pamoja na Arthritis.

Ni matumaini yangu kuwa kuanzia leo utakuwa umezifahamu faida za tunda hili.

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI