FAHAMU ZAIDI KUHUSU CHIA

FAHAMU ZAIDI KUHUSU CHIA


    Mara nyingi tumekuwa tukiyaangazia masuala mbali mbali ya vitu vinavyotuzunguka. basi Leo siyo vibaya kama tukijaribu kuziangazia afya za wenzetu.
    Na katika hili tutaongelea juu ya mbegu ndogo sana ya Chia,ambayo imeendelea
Kujipatia umaarufu siku hadi siku hivyo
Kuonekana yenye thamani sana hasa kwa
Watumiaji wake.
    Mbegu za Chia zawezakuwa na rangi Nyeupe ama Nyeusi ikiwa na michirizi ya
Mistari mfano wa ramani kwa muonekano.Ikumbukwe kuwa hakuna
Tofauti yoyote ya virutubisho kati ya Chia nyeupe na nyeusi.
    Mbegu hizi ndogo zipo na mambo mbali mbali na mengi ya kujivunia hasa
Kwa watumiaji wake.
    Katika miaka ya 3500BC,Chia ilikuwa ni
Miongoni mwa vyakula vikuu ktk kabila la
Wa Aztec chimbuko lao ikiwa ni Mexico.
Baadae miaka ya 1500 na 900BC,Chia ilikuwa tayari inalimwa na makabila mengine(Teotihuacan,Teltec).
    Tofauti na wa Aztec makabila haya mawili watu wake waliitumia Chia ktk
Matumizi mbali mbali(chakula,vinywaji baridi,shughuli za Ibada na ktk kutibu
Magonjwa mbali mbali.
   Inasemekana kuwa Wahenga ktk Nchi ya mexico na maeneo jirani waliamini kuwa mbegu za Chia zilikua na Nguvu ya ajabu.Jambo hili lilitokana haswa na uwezo wake katika kuupa Nguvu mwili wa binadamu.
   Chia ni neno linalotokana na lugha ya Mayan,likiwa na maana ya "Nguvu".Pia yasemekana kuwa mashujaa wa enzi zile kama vile Wanamichezo,Wawindaji na wapiganaji wa jadi walipata Nguvu kutoka
Katika Chia.Ivyo waliwezakukimbia(tembea)umbali mrefu zaidi bila ya kuchoka wala kuhisi njaa.

NB:Matokeo ya utafiti wa Wanasayansi
      Wanaojishughulisha na masuala ya
      Mimea na afya za binadamu yamethi-
      bitisha kuwa kijiko kimoja(tablespoon)
      Cha mbegu za Chia kipo na virutubi-
      sho vifuatavyo;...
*Omega 3(Mara 8 zaidi ya samaki
                    Salmon).
*Magnesium(32% zaidi ya broccoli).
*Iron(Mara 6 zaidi ya spinach).
*Calcium(Mara 8 zaidi y maziwa).
*Fiber(Mara nyingi zaidi ya mbegu
             katani(flaxseeds).
*Protein(Mara nyingi zaidi ya Soya).
*Potassium(64% zaidi ya Banana).
NB;PIA CHIA NI KIDHIBITI NA KIONDOA
      SUMU(Antioxidant).

FAIDA ZA KUTUMIA CHIA.

1)Inasaidia moyo kufanya kazi yake
    Vyema na kuzuia matatizo yatokanayo
     na Umri.

2)Nafaka iliyomo ndani ya mbegu ya Chia
    husaidia kufufua seli za mwili na
    kuziimarisha.

3)Kuimarisha kinga ya mwili na kuzuia
    Maradhi nyemerezi.

4)Kuimarisha Nguvu ya mwili.

5)Kusaidia matatizo ya Sukari.

6)Kuondoa tatizo la kukosa usingizi.

7)Kuondoa matatizo ya  tumbo hasa
    Wale wanaokosa haja kuu.

8)Mbegu za Chia zipo na uwezo mkubwa
   Wa kuyachoma mafuta magumu ndani
    ya Tumbo.

9)Kuboresha afya ya Ubongo.

10)Kuimarisha mifupa na kuipa Nguvu.

11)Kuondoa sumu mwilini kwa kiwango
      Cha hali ya juu.

12)Kinga dhidi ya Kansa hasa kwa
      Wanawake(breastcancer)

N.B
CHIA SEEDS HUCHANGANYWA NA
EXTRA VIGIN JUICE AU EXTRA VIGIN FOOD kwa matokeo mazuri zaidi.

       TUMIA CHIA KWA AFYA BORA .

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI

ZIJUE FAIDA KUMI (10) ZA STRAWBERRY MWILINI