FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO.
VIDONDA VYA TUMBO,DALILI NA MATIBABU YAKE
VIDONDA VYA TUMBO NINI??
>Ni kuharibika kwa ukuta wa tumbo la chakula na sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba
Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo
1. Gastric ulcers-hivi hutokea kwenye mfuko wa tumbo la chakula
2. Duodenal ulcers-hivi hutokea sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba
VISABABISHI VIKUU VYA VIDONDA VYA TUMBO
1. KUONGEZEKA KWA TINDIKALI YA HCL KWENYE TUMBO LA CHAKULA
>imekuwa ni changamoto kubwa sana kwani moja ya visababishi hivi kila siku tunakumbana navyo ndiyo maana kwa nchi kama Tanzania kutibu vidonda vya tumbo ni changamoto kubwa.
VIFUATAVYO HUONGEZA TINDIKALI YA HCL
A. Mawazo
Watu wengi tunasumbuliwa na changamoto hii ya kushambuliwa na msongo wa mawazo kila siku hii inatokana na kutojua namna ya kushughulika na msongo wa mawazo. Jifunze namna ya kuepuka msongo wa mawazo utaona mabadiliko yakitokea .
B. Madawa mbalimbali
Imekuwa ni desturi sisi kutumia dawa kama diclofenac,aspirin na zingine nyingi kama makande. Dawa hizi huzuia utengenezaji wa uteute unaolinda ukuta wa tumbo na hivyo kushambulia kwa kasi kwa ukuta wa tumbo. Pia dawa hizi huzuia utengenezwaji wa ukuta wa tumbo na hatimaye ukuta kudhoofika na kuanza kushambuliwa na tindikali. Pia dawa hizi zinaua bacteria wanao stahili kukaa tumboni yani normal flora na kufanya wadudu nyemelezi kama helicobacter pylori kushambulia ukuta wa tumbo. Kuwepo kwa walinzi hawa huyo mdudu anaye sababisha vidonda vya tumbo hata siku moja hawezi kushambuliwa. Hivyo kuwalinda bakiteria hawa ni kuhakikisha tunawalisha chakula kinachowafanya waendelee kustawi na kukulinda. Jiulize ni chakula gani kinafaa?? Jibu ni vyakula vitokanavyo na mimea na matunda hufanya bacteria walinzi wetu watulindi kwa umahili mkubwa.
C. Uvutaji wa sigara na kunywa pombe sana
D. Vyakula vibaya tunavyokuwa kila siku
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
1. Tumbo kuwaka moto sehemu ya juu kulia na endapo maumivu yakizidi husambaa hadi mgongoni.
2. Njaa hasa wakati wa usiku saa kumi na moja asubuhi utasikia tumbo linawaka moto
3. Tumbo kujaa gesi sana
4. Kichefu chefu na kuharisha kutokana na kubagua vyakula
5. Inaweza kupelekea kutapika damu,kuishiwa damu na hatimaye kifo kama mgonjwa asipo wahishwa hospitali
6. Kutoa choocheusi ni kiashiria damu inavia sehemu ya juu ya tumbo.
UKIONA DALILI KAMA HIZI TAFADHALI MUONE DAKTARI
VYAKULA VYA KUEPUKA KABISA
1. Vyakula vyenye viungo vingi.
2. Vyakula au kinywaji chenye caffeine hivyo angalia label kama wewe ni muhanga wa vyakula vya viwandani na hutaki kuacha.
3. Pombe ya aina yoyote
4. Vyakula vyote vya ngano nyeupe kama mikate nk kwani zina glutten
5. Vyakula vya sukari nyingi pia vinywaji vya sukari nyingi. Hii ni kwa sababu ulapo au unywapo sukari nyingi inalisha bakteria wabaya na hatimaye hao bacteria wazuri kufa na hawa wabaya kuanza kushambulia kuta za tumbo la chakula. Hivyo sukari huenda kulisha bacteria wabaya.
Comments
Post a Comment