FAHAMU FAIDA 6 ZA KULA TUNDA CHUNGWA

FAHAMU FAIDA 6
ZIPATIKANAZO KWA KULA TUNDA LA CHUNGWA KIAFYA.

Ukiamua kuzungumzia matunda yenye faida ndani ya mwili wa binadamu basi ni lazima utalitaja chungwa kwani lina faida muhimu ikiwemo kujenga kinga imara za mwili.

Licha kwamba baadhi ya watu hulitumia tunda hili kama kiburudisho tu bila kujua faida zake mwilini, lakini leo napenda uzifahamu hizi faida  6 unazoweza kuzipata unapokula chungwa iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.

1. UKOSEFU WA CHOO
Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe ‘fibre’, chungwa husaidia usagaji wa chakula tumboni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo.

2.HUPUNGUZA HATARI YA MAGONJWA YA MOYO
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo ‘Cardiovascular disease’

3. MIFUPA NA MENO
Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya ‘calcium’ ambayo ni muhimu kwa kuimarishaji afya ya meno.

4. AFYA YA NGOZI
‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’.

5. KINGA YA MWILI
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na malaria.

6. UGONJWA WA MAFUA
Kutokana na wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza mathalani  mafua ambayo  yanawasumbua watu wengi.

Comments

adthis

Popular posts from this blog

FAIDA ZA PILIPILI MANGA KIAFYA

FAHAMU FAIDA 10 ZA NAZI KAMA TIBA YA MWILI