Posts

Dondoo Za Afya

FAIDA ZA TANGO 1. Kuzuia kisukari, kuboresha mfumo wa damu na kuondoha kolesteroli mwilini. 2. Chanzo kikubwa cha Vitamin B. 3. Kusaidia kutunza ngozi. 4. Kuongeza maji mwilini. 5. Kukata hangover. 6. Kuimarisha mmeng'enyo wa chakula mwilini. 7. Kuzuia saratani mwilini. 8. Kusaidia kupungua uzito. 9. Kuondoa maumivu na kuboresha viungo vya mwili. 10. Kuondoa harufu mbaya ya kinywa. FAIDA ZA PAPAI 1. Kuua na kuondoa mazalia ya minyoo mwilini. 2. Kusaidia kutibu vidonda vya tumbo. 3. Kuboresha mmeng’enyo wa chakula. 4. Majani yake huleta ahueni kwa wagonjwa wa saratani. 5. Kupunguza uvimbe (anti-inflammatory). 6. Kuboresha misuli na neva mwilini. 7. Kusaidia kumeng’enya protini. 8. Kuboresha kinga ya mwili. 9. Kuboresha macho. 10. Kuboresha mfumo wa hewa FAIDA ZA UBUYU 1. Kuzuia uhalibifu na mikunjo ya ngozi. 2. Kusaidia katika kupunguza uzito wa mwili. 3. Kuimarisha moyo. 4. Kusafisha ini na kuondoa sumu. 5. Kiwango kikubwa cha vitamin C. 6. Chanzo cha m...

FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO.

Image
VIDONDA VYA TUMBO,DALILI NA MATIBABU YAKE VIDONDA VYA TUMBO NINI?? >Ni kuharibika kwa ukuta wa tumbo la chakula na sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo 1. Gastric ulcers-hivi hutokea kwenye mfuko wa tumbo la chakula 2. Duodenal ulcers-hivi hutokea sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba VISABABISHI VIKUU VYA VIDONDA VYA TUMBO 1. KUONGEZEKA KWA TINDIKALI YA HCL KWENYE TUMBO LA CHAKULA >imekuwa ni changamoto kubwa sana kwani moja ya visababishi hivi kila siku tunakumbana navyo ndiyo maana kwa nchi kama Tanzania kutibu vidonda vya tumbo ni changamoto kubwa. VIFUATAVYO HUONGEZA TINDIKALI YA HCL A. Mawazo Watu wengi tunasumbuliwa na changamoto hii ya kushambuliwa na msongo wa mawazo kila siku hii inatokana na kutojua namna ya kushughulika na msongo wa mawazo. Jifunze namna ya kuepuka msongo wa mawazo utaona mabadiliko yakitokea . B. Madawa mbalimbali  Imekuwa ni desturi sisi kutumia dawa kama diclofenac,aspirin na zing...

FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA PILIPILI

14.Pilipili kali.  Watu wengi wamekuwa wakiacha kutumia pilipili etu kwa sababu ya ukali wake. Ila itambulike kuwa ijapokuwa ni kali lakini ila faida nyingi sana kwa afya ya mtu. Pilipili pia ina vitamini c ndani yake kwa kiasi. Vitamini hivi ni muhimu sana katika mfumo mzima wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na wadudu shambulizi. Pilipili zote zina vitamin A, C na K lakini pilipili nyekundu zimezidi wenzie. Wataalamu wa afya wanazungumza kuwa antioxidant, vitamin A na C vilivyomo kwenye pilipili husaidia katika kuzuia maradhi ya saratani na baadhi ya maradhi yanayohusiana na kuzeheka, na pia husaidia katka kuboresha mfumo wa kinga. Pia vitamin K husaidia katika kuganda kwa damu, kuimarisha mifupa pia husaidia katika kulinda seli. Pilipili nyekundu ni chanzo kizuri cha carotenoid ambayo hutambulika kama lycopene, hii ni mujarabu sana katika kuzuia mwili kupata maradhi ya saratani ya kibofu, njia ya uzazi kwa kinamama na saratani ya kongosho.pia kuna carotenoid inayotambuli...

SIKU YA KUPATA MIMBA

Image

FAHAMU FAIDA ZA MBEGU ZA MABOGA

Image
FAIDA ZA MBEGU ZA MABOGA Zifuatazo ni faida za kiafya ambazo mtu anaweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga zikiwa mbichi au zilizo kaangwa: Huimarisha moyo na mifupa. Mbegu za maboga huwa kiwango kingi cha madini aina ya magnesium, ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na uimarishaji wa mifupa pamoja na mishipa ya damu sambamba  na kuongeza ufanisi wa utumbo mpana . Magnesium inaonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshtuko wa moyo na kiharusi.  Kinga ya mwili Mbegu za maboga zina kiwango cha madini aina ya zink, ambayo pia yana faida nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na na uimarishaji wa kinga mwilini , ukuaji wa seli, macho na ngozi ya mwili. Hali kadhalika zinki huimarisha nguvu za kiume. Saratani ya kibofu Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha zinki, tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu. Ugonjwa wa ini Mbegu za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na...

FAHAMU FAIDA YA KUNYWA MAJI NA KUCHANGANYA NA LIMAO

Image
FAIDA YA KUNYWA MAJI NA KUCHANGANYA NA LIMAO Umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini,lakini kunywa maji yenye ndimu na vuguvugu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku. Vitamin C nyingi iliyomo katika ndimu (au limao) ni siri ya faida za tunda hili,ukiachia vitamini C ndimu ina vitamini B-complex, madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa (apple au Zabibu). Tunajua kwa watu wengi Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi hupata tabu na baadhi ya wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na radha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida. Faida kubwa ya juisi ya ndimu ni kinga dhidi ya malaria. Kamau glasi moja ya ndimu asubuhi na mapema kabla ya kupiga mswaki na kuinywa. Hakika utakuwa umejijengea kinga dhidi ya malaria. Kisha kila siku asubuhi, kabla ya mswaki uwe na tabia ya kunywa angalau ...

FAHAMU ZAIDI KUHUSU CHIA

Image
FAHAMU ZAIDI KUHUSU CHIA     Mara nyingi tumekuwa tukiyaangazia masuala mbali mbali ya vitu vinavyotuzunguka. basi Leo siyo vibaya kama tukijaribu kuziangazia afya za wenzetu.     Na katika hili tutaongelea juu ya mbegu ndogo sana ya Chia,ambayo imeendelea Kujipatia umaarufu siku hadi siku hivyo Kuonekana yenye thamani sana hasa kwa Watumiaji wake.     Mbegu za Chia zawezakuwa na rangi Nyeupe ama Nyeusi ikiwa na michirizi ya Mistari mfano wa ramani kwa muonekano.Ikumbukwe kuwa hakuna Tofauti yoyote ya virutubisho kati ya Chia nyeupe na nyeusi.     Mbegu hizi ndogo zipo na mambo mbali mbali na mengi ya kujivunia hasa Kwa watumiaji wake.     Katika miaka ya 3500BC,Chia ilikuwa ni Miongoni mwa vyakula vikuu ktk kabila la Wa Aztec chimbuko lao ikiwa ni Mexico. Baadae miaka ya 1500 na 900BC,Chia ilikuwa tayari inalimwa na makabila mengine(Teotihuacan,Teltec).     Tofauti na wa Aztec makabila haya mawili watu wake ...

adthis