KIAFYA: HAISHAURIWI KUFANYA YAFUATAYO BAADA YA KULA CHAKULA:
1.Kuvuta sigara Kiafya mara baada ya kula chakula hairuhusiwi kuvuta sigara japo kuwa mvutaji wa siagara hupatwa na hamu kubwa ya kuvuta mara baada ya kula tabia hii huhatarisha afya, hivyo inashauriwa kusubiri angalau kwa masaa kadhaa ndipo uvute endapo ni lazima sana kwani sigara ina miliki Nikotini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, madhara yanayotokea kwa kuvuta sigara mara baada ya kula chakula ni sawa na madhara yanayotokea kwa mtu aliyevuta sigara 10 kwa mara moja na hii huchangia mtu kupata kansa ya mapafu. 2. Kula matunda Wanasayansi wamedhihirisha kuwa kiafya matunda yanatakiwa kuliwa kabla ya kula si mara baada ya kula kama ambavyo imezoeleka kwa watu wengi, Matunda yana enzymes na asali asili ambayo inahitaji kumeng’enywa ndani ya muda wa kutosha, hivyo kula matunda baada ya chakula inaweza kusababisha matatizo ya mmeng’enyo wa chakula pamoja na kiungulia. 3. Kulala Kulala mara baada ya kula ni kitendo ambacho hupendelewa kufanywa na mamilioni ya watu japokuwa tabia hii s...