VYAKULA VITAKAVYOKUONGEZEA KINGA YA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA CORONA ( COVID-19)
VYAKULA VITAKAVYOKUONGEZEA KINGA YA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA CORONA ( COVID-19) Njia za kufuata ili kuimarisha kinga ya mwili ili kupambana na maambukizi ya virusi vya corona Kwa kutambua umuhimu wa kuchukua tahadhari ya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona, nimeamua kutumia jukwaaa hili kufafanua mambo machache kuhusu kinga ya mwili (body immunity) na makundi machache ya vyakula vinavyopatikana kwa urahisi ambavyo vinauwezo wa kuongeza na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili( body immune system). Twende pamoja; 1. Hiriki Mbali na kiungo hiki kutumika kuongeza radha katika vyakula na vinywaji, hiriki ni chanzo kizuri cha madini muhimu mwilini. Madini haya ni kama vile potassium, calcium, madini ya chuma na manganese. Madini haya husaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mapafu na kuzibua mirija ya hewa, hivyo kuwapa unafuu watu wenye matatizo ya pumu na kupumua. Pia hiriki ina vitamini mbali mbali kama vile vitamin A, B na C amb...